-
Yehova Aghadhibikia MataifaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
14, 15. (a) Nchi ya Edomu na pia Jumuiya ya Wakristo zitapatwa na nini? (b) Mitajo kuhusu lami iwakayo na moshi unaopaa milele yamaanisha nini, nayo haimaanishi nini?
14 Basi, tuchunguzapo sehemu hii iliyobaki ya unabii wa Isaya, twakumbuka Edomu ya kale na Jumuiya ya Wakristo vilevile: “Vijito vyake vitageuzwa kuwa lami, na mavumbi yake yatageuzwa kuwa kiberiti, na ardhi yake itakuwa lami iwakayo.
-
-
Yehova Aghadhibikia MataifaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Nchi ya Edomu yawa ukiwa kabisa hivi kwamba mavumbi ni kama kiberiti na mabonde yamejaa lami, wala si maji. Kisha vifaa hivyo vinavyoweza kuwaka rahisi vyawashwa moto!—Linganisha Ufunuo 17:16.
15 Wengine wana maoni ya kwamba moto, lami, na kiberiti zinazotajwa ni uthibitisho wa kuwapo kwa helo ya moto. Lakini Edomu haitupwi ndani ya moto unaowaziwa kuwa helo ili ichomeke milele. Badala yake, hiyo yaharibiwa, ikitoweka kutoka ulimwenguni kana kwamba imechomwa kabisa kwa moto na kiberiti. Kama unabii uendeleavyo kuonyesha, tokeo la mwisho si mateso ya milele, bali “ukiwa . . . utupu . . . si kitu.” (Isaya 34:11, 12)
-