-
Yehova Mungu Awarehemu MabakiUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, BWANA ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa Sitara.”—Isaya 4:4, 5.
-
-
Yehova Mungu Awarehemu MabakiUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
20. (a) Semi “wingu,” “moshi,” na “miali ya moto” zatukumbusha nini? (b) Kwa nini haitawabidi wahamishwa hao waliotakaswa kuogopa?
20 Yehova, kupitia Isaya, aahidi kwamba atawatunza kwa upendo mabaki hao waliotakaswa. Semi “wingu,” “moshi,” na “miali ya moto” zatukumbusha jinsi Yehova alivyowatunza Waisraeli baada ya kuondoka Misri. “Nguzo ya moto na ya wingu” iliwalinda dhidi ya Wamisri waliokuwa wakiwaandama; hiyo pia iliwaongoza nyikani. (Kutoka 13:21, 22; 14:19, 20, 24) Yehova alipojidhihirisha katika Mlima Sinai, mlima huo “wote pia u[li]toa moshi.” (Kutoka 19:18) Basi, haitawabidi wahamishwa hao waliotakaswa kuogopa. Yehova atakuwa Mlinzi wao. Atakuwa pamoja nao wakusanyikapo katika makao yao wenyewe au wakusanyikapo kwenye mikusanyiko mitakatifu.
-