Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mungu wa Kweli Anatabiri Ukombozi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Maelezo ya kifungu hicho yanafikia upeo wenye kuvutia sana hatua kwa hatua kwa kutangaza jina la mwanamume atakayekomboa taifa hilo kutoka Babiloni.

  • Mungu wa Kweli Anatabiri Ukombozi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.”—Isaya 44:24-28.

  • Mungu wa Kweli Anatabiri Ukombozi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 22. Eleza Mto Eufrati unakauka jinsi gani.

      22 Kwa kawaida waaguzi wasiopuliziwa hawathubutu kutabiri mambo hususa, kwa kuhofu kwamba watathibitishwa kuwa waongo baada ya muda. Lakini Yehova ni tofauti kwa sababu anafunua kupitia Isaya jina hususa la mwanamume ambaye Yeye atamtumia kuwaweka huru watu wake watoke utekwani, waweze kwenda nyumbani wakajenge upya Yerusalemu na hekalu. Jina lake ni Koreshi, na anajulikana kuwa Koreshi Mkuu wa Uajemi.

  • Mungu wa Kweli Anatabiri Ukombozi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 23. Kuna maandishi gani ya kuonyesha utimizo wa ule unabii wa kwamba Koreshi angekomboa Israeli?

      23 Namna gani ile ahadi ya kwamba Koreshi atawafungua watu wa Mungu na kwamba atahakikisha Yerusalemu na hekalu vitajengwa upya? Koreshi mwenyewe, katika tangazo rasmi lililohifadhiwa katika Biblia, anatangaza hivi: “Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, BWANA, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya BWANA, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu.” (Ezra 1:2, 3) Ahaa! Neno la Yehova kupitia Isaya limetimizwa kabisa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki