-
Yule Mwanamke Tasa AshangiliaUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Milima yaweza kutoweka, vilima vyaweza kuondolewa, lakini fadhili zangu hazitakuondoka, agano langu la amani halitaondolewa. Mimi Mwenyezi-Mungu nikuhurumiaye nimesema.” (Isaya 54:9, 10, “BHN”)
-
-
Yule Mwanamke Tasa AshangiliaUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
20 Inafariji kujua kwamba adhabu ambayo ni lazima iwapate—ule uhamisho wa miaka 70 katika Babiloni—itatukia mara moja tu. Ikimalizika, haitatukia tena. Baada ya hapo, ‘agano la Mungu la amani’ litaanza kutumika. Neno la Kiebrania la “amani” halimaanishi kutokuwako kwa vita tu bali pia “hali njema ya kila aina.” Kwa upande wa Mungu, agano hilo ni la kudumu. Vilima na milima inaweza kutoweka kwa urahisi kuliko fadhili za upendo wa Mungu kuelekea watu wake waaminifu. Lakini inasikitisha kwamba hatimaye taifa lake la kidunia litashindwa kutimiza upande wao wa agano hilo, livunje-vunje amani yake lenyewe kwa kumkataa Mesiya. Hata hivyo, wana wa “Yerusalemu la juu” walifanya vema zaidi. Kipindi chao kigumu cha nidhamu kilipomalizika, walikuwa na uhakikisho wa kulindwa na Mungu.
-