Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Ahuisha Roho ya Wanyenyekevu
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Utakapolia, na wakuponye hao uliowakusanya; lakini upepo utawachukua; uvuvio tu utawachukulia mbali.” (Isaya 57:12, 13a)

  • Yehova Ahuisha Roho ya Wanyenyekevu
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • ‘Hao aliowakusanya,’ maana yake sanamu zake nyingi, hawatamponya. Maafa yatakapotokea ghafula, miungu anayoitumaini itapeperushwa mbali kwa pumzi moja tu.

      15 Maneno ya Yehova yanatimizwa mwaka wa 607 K.W.K. wakati Mfalme Nebukadreza wa Babiloni anapoharibu Yerusalemu, anachoma hekalu kwa moto na kuteka idadi kubwa ya watu. “Hivyo Yuda wakachukuliwa utumwani kutoka nchi yao.”—2 Wafalme 25:1-21.

      16. Ni nini kinachoingoja Jumuiya ya Wakristo na sehemu nyinginezo za “Babiloni Mkubwa”?

      16 Vivyo hivyo, sanamu chungu nzima za Jumuiya ya Wakristo hazitamkomboa katika siku ya hasira ya Yehova. (Isaya 2:19-22; 2 Wathesalonike 1:6-10) Jumuiya ya Wakristo itaangamizwa kabisa pamoja na sehemu nyingine zote za “Babiloni Mkubwa,” ile milki ya ulimwengu ya dini za uwongo. Hayawani wa mfano mwenye rangi nyekundu nyangavu na pembe zake kumi ‘watamfanya Babiloni Mkubwa awe ukiwa na uchi, na watakula kabisa sehemu zake zenye nyama na watamchoma kabisa kwa moto.’ (Ufunuo 17:3, 16, 17) Sisi tunafurahi kama nini kwamba tumetii amri hii: “Tokeni kwake, watu wangu, ikiwa hamtaki kushiriki pamoja naye dhambi zake, na ikiwa hamtaki kupokea sehemu ya tauni zake”! (Ufunuo 18:4, 5) Tusirudi kwake wala kwenye njia zake kamwe.

      ‘Atakayekimbilia Usalama Kwangu Ataimiliki Nchi’

      17. ‘Mwenye kukimbilia usalama kwa Yehova’ anapewa ahadi gani, na inatimizwa lini?

      17 Namna gani maneno yanayofuata ya unabii wa Isaya? “Watakaokimbilia usalama kwangu, wataimiliki nchi, mlima wangu mtakatifu utakuwa mali yao.” (Isaya 57:13b, “BHN”) Yehova anaongea na nani sasa? Anaeleza mambo yatakayotokea baada ya yale maafa makubwa yanayokuja, na anatabiri kwamba watu wake watakombolewa kutoka Babiloni kisha ibada safi irudishwe katika mlima wake mtakatifu, Yerusalemu. (Isaya 66:20; Danieli 9:16) Hiki ni kitia-moyo kweli kweli kwa Wayahudi wowote wanaobaki wakiwa waaminifu!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki