-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Maana ajaye kupigana naye atatenda kadiri apendavyo, walahapana mtu atakayesimama mbele yake; naye atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi mwake.”—Danieli 11:15, 16.
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Alitenda “kadiri apendavyo” kwa sababu majeshi ya mfalme wa kusini wa Misri hayakuweza kusimama mbele yake. Kisha Antiochus wa Tatu akapiga mwendo kuelekea Yerusalemu, jiji kuu la “nchi ya uzuri,” Yuda. Mwaka wa 198 K.W.K., Yerusalemu na Yuda ziliacha kutawalwa na mfalme wa kusini wa Misri na kuanza kutawalwa na mfalme wa kaskazini wa Siria. Naye Antiochus wa Tatu, mfalme wa kaskazini, akaanza ‘kusimama katika nchi ya uzuri.’ Mlikuwemo ‘uharibifu mikononi mwake’ kwa Wayahudi wote na Wamisri wote waliompinga.
-