Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wafalme Wawili Wapambana
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 34, 35. (a) Mfalme wa kaskazini aliuelekeza uso wake kwenye ‘nchi zipi za pwani’? (b) Roma ilikomeshaje “aibu” kutoka kwa mfalme wa kaskazini? (c) Antiochus wa Tatu alikufaje, na mfalme wa kaskazini aliyefuata alikuwa nani?

      34 Malaika alisema hivi akirejezea kushindwa huko kwa mfalme wa kaskazini: “Baada ya hayo [Antiochus wa Tatu] atauelekeza uso wake kwenye visiwa, naye atavipiga visiwa vingi [“nchi nyingi za pwani na kuzishinda,” BHN]; lakini mkuu mmoja [Roma] ataikomesha aibu iliyoletwa na yeye [Roma]; naam, aibu yake [kutoka kwa Antiochus wa Tatu] hiyo [Roma] atamrudishia mwenyewe.

  • Wafalme Wawili Wapambana
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 35 ‘Nchi hizo za pwani’ ni Makedonia, Ugiriki, na Asia Ndogo. Vita vilizuka Ugiriki mwaka wa 192 K.W.K., na Antiochus wa Tatu akashawishiwa aende Ugiriki. Hatimaye Roma ikatangaza vita dhidi yake kwa kuwa ilikasirishwa na jitihada za mfalme wa Siria za kuteka maeneo zaidi huko. Huko Thermopylae alishindwa na Waroma. Mwaka mmoja hivi baada ya kushindwa katika vita ya Magnesia mwaka wa 190 K.W.K., alilazimika kuacha kila kitu huko Ugiriki, Asia Ndogo, na maeneo yaliyo magharibi mwa Milima Taurus. Roma ilimtoza faini kubwa na kusitawisha utawala wake juu ya mfalme wa kaskazini wa Siria. Akiwa amefukuzwa kutoka Ugiriki na Asia Ndogo na baada ya kupoteza karibu meli zake zote, Antiochus wa Tatu ‘aliuelekeza uso wake mwenyewe kwenye ngome za nchi yake mwenyewe,’ Siria. Waroma walikuwa ‘wamemrudishia aibu yake mwenyewe.’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki