-
Aokolewa Asiliwe na Simba!Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
NJAMA YA UUAJI YAANZA KUTEKELEZWA
7. Mawaziri na maliwali walimpendekezea mfalme nini, nao walifanyaje hivyo?
7 Dario alifikiwa na msafara wa mawaziri na maliwali ‘waliokusanyika pamoja mbele ya mfalme.’ Usemi wa Kiaramu unaotumiwa hapa una wazo la rabsharabsha zenye kelele. Yaonekana kwamba watu hao walifanya ionekane kana kwamba walikuwa na jambo la dharura la kumwambia Dario. Huenda walifikiri kwamba hangezusha maswali juu ya pendekezo lao ikiwa wangemwambia kwa usadikisho na kana kwamba ni jambo lililohitaji kuchukuliwa hatua mara moja.
-