Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Njia za Yehova Zimenyooka”
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Novemba 15
    • 9, 10. Andiko la Hosea 11:1-4 liliwahusuje Waisraeli?

      9 Tunaweza kuwa na uhakika kwamba sikuzote Yehova huwatendea watu wake kwa upendo. Uthibitisho wa jambo hilo unapatikana katika Hosea 11:1-4, ambapo tunasoma hivi: “Israeli alipokuwa mvulana, ndipo nikampenda, na kutoka Misri nilimwita mwanangu. . . . Wakaanza kutoa dhabihu kwa sanamu za Baali, nao wakaanza kufukiza moshi wa dhabihu kwa sanamu za kuchongwa. Lakini mimi, nilimfundisha Efraimu [Waisraeli] kutembea, nikawachukua mikononi mwangu; wala hawakutambua kwamba nilikuwa nimewaponya.

  • “Njia za Yehova Zimenyooka”
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Novemba 15
    • 10 Katika andiko hilo, Waisraeli wanalinganishwa na mtoto mchanga. Yehova aliwafundisha Waisraeli kutembea, akawachukua mikononi mwake. Naye alizidi kuwavuta kwa “kamba za upendo.” Mfano huo unavutia kama nini! Wazia kwamba wewe ni mzazi nawe unamsaidia mtoto wako mchanga atembee kwa mara ya kwanza. Unanyoosha mikono yako.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki