Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Igeni Rehema ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
    • Kwa kujibu akamwambia baba yake, ‘Hii ni miaka mingi sana ambayo mimi nimekutumikia wewe kama mtumwa na kamwe hata mara moja sijakiuka amri yako, na bado kamwe hata mara moja hukunipa mwana-mbuzi ili mimi nijifurahishe mwenyewe pamoja na marafiki wangu.

  • Igeni Rehema ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
    • —Luka 15:28-30.

  • Igeni Rehema ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
    • 8 Kwa maneno hayo, ndugu ya mwana mpotevu alionyesha wazi kwamba alikuwa ameshindwa kuelewa maana halisi ya uana. Alimtumikia baba yake sawa na vile mwajiriwa anavyomtumikia mwajiri wake. Kama alivyomwambia baba yake: “Nimekutumikia wewe.” Ni kweli, mwana huyu mwenye umri mkubwa zaidi hakuwa amewahi kuondoka nyumbani au kukiuka amri ya baba yake. Lakini utii wake ulichochewa na upendo? Je, alipata shangwe ya kweli katika kumtumikia baba yake, au badala yake hatua kwa hatua alikuwa amekuwa mwenye kuridhika mno, akijiamini kuwa mwana mwema kwa sababu tu alitimiza wajibu wake mbalimbali “katika shamba”?

  • Igeni Rehema ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
    • 9. Eleza jinsi viongozi Wayahudi walivyofanana na mwana mwenye umri mkubwa zaidi.

      9 Viongozi wa kidini Wayahudi walifanana na mwana huyo mwenye umri mkubwa zaidi. Waliamini kwamba walikuwa waaminifu-washikamanifu kwa Mungu kwa sababu walishikamana kabisa na mfumo wa sheria. Ni kweli, utii ni muhimu. (1 Samweli 15:22) Lakini kukazia kwao matendo kupita kiasi kuligeuza ibada ya Mungu ikawa kawaida isiyo na hisia, wonyesho wa nje tu wa ujitoaji usio na hali ya kiroho ya kweli. Akili zao zilijawa na mapokeo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki