Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jinsi ya Kujilinda Dhidi ya Ulaghai
    Amkeni!—2004 | Julai 22
    • Je, una anwani ya barua-pepe? Ikiwa ndivyo, huenda ukapokea matangazo ya biashara kutoka kwa watu usiowajua. Ijapokuwa matangazo hayo huonyesha bidhaa na huduma nyingi zinazotolewa, mengi ni ya ulaghai. Ukijibu barua-pepe ya mtu usiyemjua kwa kutuma pesa kwa ajili ya bidhaa au huduma fulani, huenda usipate chochote. Hata ukipokea kitu, hakitalingana na pesa ulizotuma. Usinunue chochote kutoka kwa mtu usiyemjua ambaye anakutumia ujumbe wa barua-pepe.

  • Jinsi ya Kujilinda Dhidi ya Ulaghai
    Amkeni!—2004 | Julai 22
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 8, 9]

      Mbinu Sita Zinazotumiwa Kwenye Barua-pepe

      1. Biashara za kuwatafuta washiriki wapya: Biashara hizo huonwa kuwa njia ya kujitajirisha bila jitihada yoyote wala kutumia pesa nyingi. Watu wengine hupewa kompyuta au kifaa kingine cha elektroni wanapolipa pesa za kujiunga na biashara hizo na kutafuta washiriki wengine. Wakati mwingine watu hutumiwa barua zenye orodha ya majina. Mara nyingi barua hizo si halali. Watu wengi wanaojiingiza katika biashara hizo hupoteza pesa zao.

      2. Mbinu za kujitengenezea vitu nyumbani: Njia moja inahusisha kuwapa watu kazi ya kutengeneza vito, vitu vya watoto vya kuchezea, au bidhaa nyinginezo. Watu hutumia pesa na wakati mwingi kununua vifaa vya kutengeneza vitu hivyo na kuvitengeneza, lakini mwishowe wenye biashara wanakataa kuvinunua kwa sababu wanaviona kuwa havifai.

      3. Mbinu zinazohusu afya na lishe: Kuna matangazo mengi ya biashara kwenye Intaneti kuhusu bidhaa mbalimbali, kama vile dawa zinazomsaidia mtu kupunguza uzito bila kuhitaji kufanya mazoezi au kubadili mazoea ya kula, dawa za kuongeza nguvu za kujamiiana, na krimu za kuzuia upara. Nyakati nyingine matangazo hayo huambatana na maelezo ya wanunuzi ambao wanasifu bidhaa hizo. Baadhi ya misemo inayotumiwa mara nyingi katika matangazo hayo ni kama vile “hatua kubwa ya kisayansi,” “dawa ya magonjwa yote,” na “siri ya mafanikio.” Ukweli ni kwamba nyingi ya bidhaa hizo hazifanyi kazi.

      4. Nafasi za kutega uchumi: Katika mbinu hii, watu huahidiwa watapata faida kubwa bila hasara au hatari zozote. Mbinu inayotumiwa sana inahusisha kutega uchumi katika benki iliyo katika nchi nyingine. Watu wanaotega uchumi hushawishiwa kwa kuhakikishiwa kwamba wale wanaoshughulika na pesa zao wana uhusiano na mashirika makubwa na wana habari muhimu.

      5. Kuondolewa lawama: Katika mbinu hii, watu huahidiwa kwamba habari zisizofaa kuwahusu zitaondolewa kwenye rekodi zao za biashara ili waweze kupata kadi ya mkopo, mkopo wa kununua gari, au wapate kazi. Ijapokuwa wanatoa ahadi nyingi, watu wanaofanya biashara hizo hawazitekelezi.

      6. Kujishindia likizo: Katika mbinu hii, mtu hupata ujumbe wa barua-pepe unaompongeza kwa kujishindia likizo ya bei nafuu. Ujumbe mwingine husema kwamba ni wewe tu uliyechaguliwa kati ya wengi. Inafaa kukumbuka kwamba huenda mamilioni ya watu wametumiwa ujumbe huo na huduma utakazopata zitakuwa duni zikilinganishwa na yale yaliyosemwa katika matangazo yao.

      [Hisani]

      Source: U.S. Federal Trade Commission

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki