-
Mahali Ambako Ibada ya Kweli na Upagani IlitofautianaMnara wa Mlinzi—2004 | Desemba 15
-
-
Hekalu la Artemi Laporomoka
Madhehebu ya Artemi yalikuwa yametia mizizi huko Efeso. Kabla Mfalme Croesus kuanza kutawala, mungu-mke Cybele ndiye aliyekuwa mungu mkuu katika eneo hilo. Kwa kudai kwamba Cybele alikuwa na uhusiano wa kiukoo na miungu ya Kigiriki, Croesus alitumaini kuanzisha ibada ya mtu ambaye angeabudiwa na Wagiriki na wasio Wagiriki. Kwa msaada wake, kazi ya kujenga hekalu la Artemi, aliyekuwa mrithi wa Cybele, ilianza katikati mwa karne ya sita K.W.K.
Kujengwa kwa hekalu hilo kulikuwa hatua muhimu katika ustadi wa kujenga wa Wagiriki. Kabla ya hapo, hakuna jengo kama hilo lililojengwa kwa vipande vikubwa vya marumaru na lenye ukubwa kama huo lililopata kujengwa. Hekalu hilo liliharibiwa kwa moto mwaka wa 356 K.W.K. Watu wengi walipata kazi na pia mahujaji walitembelea hekalu lililojengwa upya na lenye fahari kama lile la kwanza. Hekalu hilo lenye upana wa meta 50 hivi na urefu wa meta 105 lilijengwa kwenye eneo lililoinuka lenye upana wa meta 73 hivi na urefu wa meta 127. Lilionwa kuwa mojawapo ya maajabu saba ya ulimwengu. Hata hivyo, si kila mtu aliyependezwa nalo. Mwanafalsafa Heracleitus wa Efeso alifananisha njia yenye giza iliyoelekea kwenye madhabahu na giza la kiadili, naye aliona maadili ya hekalu kuwa mabaya zaidi kuliko ya wanyama. Hata hivyo, wengi waliona kwamba patakatifu pa Artemi huko Efeso hapangeporomoka kamwe. Historia ilionyesha jambo lililo kinyume na hilo. Kitabu Ephesos—Der neue Führer (Efeso—Mwongozo Mpya) kinasema: “Kufikia karne ya pili, ibada ya Artemi na ya miungu mingine iliporomoka kwa ghafula.”
Katika karne ya tatu W.K., Efeso lilikumbwa na tetemeko kubwa la nchi. Isitoshe, vitu vyenye thamani na vyenye kuvutia ambavyo vilikuwa katika hekalu la Artemi viliporwa na mabaharia Wagothi kutoka Bahari Nyeusi, ambao waliteketeza hekalu hilo. Kitabu kilichotangulia kutajwa kinasema: “Artemi angeendeleaje kuonwa kuwa mlinzi wa jiji na hali hakuweza kulinda makao yake mwenyewe?”—Zaburi 135:15-18.
Mwishowe, kuelekea mwisho wa karne ya nne W.K., Maliki Theodosius wa Kwanza alitangaza “Ukristo” kuwa dini rasmi. Upesi kuta za hekalu la Artemi ambalo wakati mmoja lilikuwa maarufu zikawa machimbo ya vifaa vya kujengea. Ibada ya Artemi ikapoteza umashuhuri kabisa. Shahidi mmoja asiyetajwa jina alisema hivi kuhusu shairi fupi la kutukuza hekalu hilo kuwa mojawapo ya maajabu ya ulimwengu wa kale: “Sasa limekuwa mahali penye ukiwa na penye kuaibisha zaidi.”
-
-
Mahali Ambako Ibada ya Kweli na Upagani IlitofautianaMnara wa Mlinzi—2004 | Desemba 15
-
-
[Picha katika ukurasa wa 27]
Magofu ya hekalu la Artemi
-