Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Linda Ngozi Yako!
    Amkeni!—2005 | Juni 8
    • Australia ina kiwango cha juu cha visa vya ugonjwa wa kansa ya ngozi, hasa ile inayoathiri chembe za ndani za ngozi.b Hii ni kwa sababu wakazi wengi wa nchi hiyo ambao walihama kutoka Ulaya Kaskazini wana ngozi yenye rangi hafifu, na wengi wao huishi pwani yenye fuo zenye jua. Uchunguzi waliofanyiwa wahamiaji hao unadokeza kwamba wale wanaohamia Australia wakiwa wachanga hukabili hatari kubwa zaidi ya kupatwa na kansa inayoathiri chembe za ngozi za ndani, jambo linaloonyesha umuhimu wa kujifunza tangu utotoni kuhusu madhara ya kupigwa na jua. Serikali ya Australia imeanzisha kampeni kali ya kuwafunza watu kuhusu hatari za jua kwa kuwaambia wavae t-shati, kofia, na kujipaka losheni ya kujikinga na jua. Mabadiliko hayo madogo katika mtindo wa maisha yamekuwa na matokeo makubwa katika kuzuia kansa inayoathiri chembe za ndani za ngozi kati ya vijana nchini humo.

  • Linda Ngozi Yako!
    Amkeni!—2005 | Juni 8
    • b Kulingana na Baraza la Kansa la New South Wales, “Mwaustralia mmoja kati ya wawili atapatwa na aina fulani ya kansa ya ngozi maishani mwake.” Huko Queensland, Australia, mnamo mwaka wa 1998, mtu 1 kati ya watu 15 alikabili hatari ya kupatwa na kansa inayoathiri chembe za ndani za ngozi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki