-
Je, Utafune Tambuu?Amkeni!—2012 | Februari
-
-
Zoea Lenye Madhara
“Popoo zimekuwa zikitafunwa tangu zamani na zimetumiwa hasa kwa sababu za kijamii, kitamaduni, na kidini,” inasema ripoti moja katika jarida Oral Health. “Mara nyingi watafunaji huona zoea hilo kuwa halina madhara na husema kwamba wanajihisi wakiwa na afya, msisimuko, [na] kuhisi joto mwilini . . . Hata hivyo, kuna uthibitisho kwamba zoea hilo lina madhara.” Madhara gani?
Mashirika ya kuzuia matumizi ya dawa za kulevya yanasema kwamba mojawapo ya kemikali zilizo katika tambuu inaweza kufanya mtu awe mraibu. Kwa kweli, watafunaji fulani hutafuna kokwa 50 hivi za mpopoo kwa siku! Muda si muda, meno hugeuka rangi, na huenda wakawa na ugonjwa wa fizi. Jarida Oral Health, linasema kwamba kwa wale wanaotafuna tambuu kwa ukawaida, huenda utando wao wenye ute ulio ndani ya kinywa ukageuka na kuwa na rangi ya kahawia na kunyauka. Huenda pia wakapata makovu mdomoni.
Kutafuna tambuu pia kunahusianishwa na aina fulani ya kansa ya mdomo, ambayo pia inaweza kutokea nyuma ya koo. Visa vingi vya kansa ya mdomo miongoni mwa watu wazima huko Kusini-Mashariki mwa Asia vinathibitisha jambo hilo. Nchini Taiwan, asilimia 85 hivi ya kansa za mdomo huripotiwa kati ya watu wanaotafuna tambuu. Isitoshe, “visa vya kansa ya mdomo nchini Taiwan—ambayo ni moja kati ya magonjwa 10 yanayosababisha vifo katika kisiwa hicho—vimeongezeka mara nne hivi katika miaka 40 iliyopita,” linasema gazeti The China Post.
Hali iko hivyo sehemu nyingine. Gazeti Papua New Guinea Post-Courier linasema: “Tambuu ambayo wakazi wengi wa Papua New Guinea wanapenda kutafuna, huwaua watu 2,000 hivi kwa mwaka na husababisha matatizo mengine mengi ya afya, linasema Shirika la Kitiba la PNG.” Daktari mmoja ambaye pia huandika makala za kitiba anasema: “Madhara yanayotokana na kutafuna tambuu kwa muda mrefu . . . ni mengi kama yale ya uvutaji sigara,” na yanatia ndani magonjwa ya moyo.
-
-
Je, Utafune Tambuu?Amkeni!—2012 | Februari
-
-
[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 23]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Zoea la kutafuna tambuu linaweza kusababisha matatizo hatari ya afya
Meno yaliyogeuka rangi na ugonjwa wa fizi
Makovu ndani ya mdomo
Kansa ya mdomo
-