Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Dhamiri Yako Imezoezwa Vizuri?
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Oktoba 1
    • Hivyo, tunapokabili suala au uamuzi fulani, tunapaswa kwanza kufikiria kanuni za Biblia ambazo huenda zikahusika. Baadhi ya kanuni hizo huenda ni: kuheshimu ukichwa (Wakolosai 3:18, 20); unyoofu katika mambo yote (Waebrania 13:18); kuchukia lililo baya (Zaburi 97:10); kufuatia amani (Waroma 14:19); kutii wenye mamlaka (Mathayo 22:21; Waroma 13:1-7); kujitoa kabisa kwa Mungu (Mathayo 4:10); kutokuwa sehemu ya ulimwengu (Yohana 17:14); kuepuka mashirika mabaya (1 Wakorintho 15:33); kuwa na kiasi katika mavazi na mapambo (1 Timotheo 2:9, 10); na kutowakwaza wengine (Wafilipi 1:10). Hivyo, kutambua kanuni muhimu za Biblia kunaweza kuimarisha dhamiri yetu na kutusaidia kufanya maamuzi yafaayo.

  • Je, Dhamiri Yako Imezoezwa Vizuri?
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Oktoba 1
    • Unapofanya maamuzi, tafuta mwongozo wa Mungu. (Yakobo 1:5) Jifunze Neno la Mungu, na uache kanuni zake zifinyange akili na moyo wako. (Methali 2:3-5) Mambo mazito yanapotokea, zungumza na Wakristo wakomavu ili uwe na hakika kwamba unaelewa vizuri kanuni za Biblia zinazohusika. (Methali 12:15; Waroma 14:1; Wagalatia 6:5) Fikiria jinsi uamuzi wako utakavyoathiri dhamiri yako, jinsi utakavyowaathiri wengine, na la muhimu zaidi, jinsi utakavyoathiri uhusiano wako pamoja na Yehova.—1 Timotheo 1:5, 18, 19.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki