Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Biblia Yafanywa Kuwa Buku Moja
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Mei 1
    • Tumeathiriwaje na Codex Grandior? Tangu wakati wa Cassiodorus, wanakili na wachapaji wamependelea sana kuitoa Biblia ikiwa buku moja moja. Hata wakati huu, kuwa na Biblia ikiwa buku moja kumefanya iwe rahisi watu kuisoma na hivyo kunufaika na nguvu zake maishani mwao.—Waebrania 4:12.

  • Biblia Yafanywa Kuwa Buku Moja
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Mei 1
    • [Ramani katika ukurasa wa 29]

      (Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

      Safari ya Codex Grandior

      Vivarium makao ya watawa

      Roma

      Jarrow

      Wearmouth

  • Biblia Yafanywa Kuwa Buku Moja
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Mei 1
    • Flavius Magnus Aurelius Cassiodorus alizaliwa katika familia tajiri wapata mwaka wa 485-490 W.K. huko Calabria, kwenye ncha ya kusini mwa Italia ya leo. Aliishi kipindi chenye msukosuko sana katika historia ya Italia wakati ambapo nchi hiyo inayozungukwa na maji ilikaliwa kwanza na Wagothi, kisha na watu wa Byzantium. Alipokuwa na umri wa miaka 60 au 70 hivi, Cassiodorus alianzisha makao ya watawa ya Vivarium na maktaba karibu na makao yake huko Squillace, Calabria.

      Mhariri Makini wa Biblia

      Mojawapo ya mambo ambayo Cassiodorus alihangaikia zaidi ya yote ni jinsi ambavyo Biblia ingeweza kufikia watu. Mwanahistoria Peter Brown aandika, “kulingana na maoni ya Cassiodorus, vichapo vyote vya Kilatini vingetumiwa ili kufanya Maandiko yapatikane kwa watu. Vifaa vyote vilivyokuwa vimetumiwa hapo awali kujifunza na kunakili maandishi ya kale vingetumiwa ili kuyafahamu Maandiko na kuyanakili kwa busara. Utamaduni wote wa Kilatini ulipasa kuzunguka jua kubwa la Neno la Mungu kama vile mfumo wa nyota ambao umetoka tu kubuniwa.”

      Cassiodorus aliwakusanya watafsiri na wanasarufi kwenye makao ya watawa ya Vivarium kusudi waunganishe vitabu vyote vya Biblia. Yeye ndiye aliyesimamia kazi iliyohitaji umakini mkubwa kuhusiana na uhariri. Aliwapa kazi hiyo wanaume wachache wenye elimu. Wanaume hao wangepaswa kuepuka kusahihisha harakaharaka mambo yaliyodhaniwa kuwa makosa ya waandishi. Ikiwa walikuwa na swali kuhusiana na sarufi, hati za kale za Biblia ndizo zingekuwa zenye kutegemeka zaidi kuliko matumizi ya kawaida ya Kilatini. Cassiodorus alitoa agizo hili: “Matumizi ya kisarufi yasiyo ya kawaida . . . yapasa kuhifadhiwa, kwa kuwa si rahisi kupotosha maandiko yanayotambuliwa kuwa yalipuliziwa. . . . Lazima njia ambayo Biblia inatumia semi fulani, mifano, na misemo, ihifadhiwe, hata ikiwa njia hiyo yaonekana kuwa isiyo ya kawaida kulingana na viwango vya lugha ya Kilatini. Majina ya ‘Kiebrania’ pia yapasa kuhifadhiwa.”—The Cambridge History of the Bible.

      Maandishi ya Codex Grandior

      Wanakili kwenye makao ya watawa ya Vivarium walipewa kazi ya kunakili nakala tatu tofauti za Biblia katika Kilatini. Labda mojawapo ya nakala hizo, ambayo ilikuwa na mabuku tisa, iliandikwa kwa Kilatini cha zamani. Nakala hiyo ilinakiliwa mwishoni mwa karne ya pili. Nakala ya pili ilikuwa ile ya Vulgate ya Kilatini, iliyokamilishwa na Jerome mwanzoni mwa karne ya tano. Nakala ya tatu, Codex Grandior, yaani “codex kubwa zaidi” ilinakiliwa kutoka katika Biblia tatu. Nakala hizi mbili za mwisho, Vulgate na Codex Grandior, ziliunganisha pamoja vitabu vyote vya Biblia kuwa buku moja.

      Yaonekana Cassiodorus ndiye aliyekuwa wa kwanza kuunganisha Biblia za Kilatini kuwa buku moja moja, na kuziita pandectae.a Bila shaka alitambua kwamba lilikuwa jambo la busara kuunganisha vitabu vyote vya Biblia kuwa buku moja, hivyo usomaji wa Biblia ukawa jambo lisilochukua muda mwingi.

      Kutoka Kusini mwa Italia Hadi Visiwa vya Uingereza

      Muda mfupi baada ya kifo cha Cassiodorus (yapata mwaka wa 583 W.K.), Codex Grandior ilianza kusafirishwa. Wakati huo, inaaminika kwamba vitabu fulani vya maktaba ya Vivarium vilikuwa vimehamishwa na kupelekwa kwenye maktaba ya Lateran huko Roma. Katika mwaka wa 678 W.K., mkuu wa makao ya watawa wanaume Ceolfrith, aliyekuwa Mwingereza, alikuja na codex hiyo kwenye Visiwa vya Uingereza aliporudi kutoka Roma alikokaa kwa muda fulani. Hivyo, codex hiyo ikaletwa kwenye makao ya watawa ya Wearmouth na Jarrow, ambayo yalisimamiwa na Ceolfrith. Makao hayo yalikuwa katika eneo ambalo sasa ni Northumbria, Uingereza.

  • Biblia Yafanywa Kuwa Buku Moja
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Mei 1
    • Ile Codex Grandior ya kwanza ambayo Cassiodorus aliagiza inakiliwe imepotea.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki