Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Aprili 1
    • Hilo ndilo tatizo lililomkabili mtafsiri wa Biblia Robert Moffat. Mwaka wa 1821, akiwa na umri wa miaka 25, Moffat alianzisha misheni miongoni mwa watu kusini mwa Afrika wenye kusema Kitswana. Ili ajifunze lugha yao isiyoandikwa, alichangamana na hao watu. Moffat alidumu na, bila msaada wa vijitabu vya masomo ya kwanza au kamusi, hatimaye akaijua kabisa hiyo lugha, akasitawisha namna ya kuiandika na kuwafundisha Watswana fulani kuisoma hati hiyo. Mwaka wa 1829, baada ya kufanya kazi miongoni mwa Watswana kwa miaka minane, alimaliza kutafsiri Gospeli ya Luka. Baadaye alisema hivi: “Nimejua juu ya watu ambao wamekuja mamia ya kilometa ili kujipatia nakala za [Gospeli ya] Mtakatifu Luka. . . . Nimewaona wakipokea sehemu za [Gospeli ya] Mtakatifu Luka, na kutoa machozi juu yazo, na kuzishika kifuani, na kububujika machozi ya shukrani, mpaka nikasema kwa zaidi ya mmoja, ‘Utaviharibu vitabu vyako kwa machozi yako.’” Moffat pia alisema juu ya mwanamume mmoja Mwafrika aliyeona watu kadhaa wakiisoma Gospeli ya Luka na kuwauliza walichokuwa wamepata. “Ni neno la Mungu,” wakajibu. “Je, hilo husema?” huyo mwanamume akauliza. “Ndiyo,” wakasema, “hilo husema na moyo.”

      14 Watafsiri wenye kujitoa kama Moffat waliwapa Waafrika wengi fursa yao ya kwanza ya kuwasiliana katika maandishi. Lakini watafsiri waliwapa Waafrika zawadi yenye thamani hata zaidi—Biblia katika lugha yao wenyewe. Isitoshe, Moffat alitokeza lile jina la Mungu kwa Watswana, naye alilitumia jina hilo kotekote katika tafsiri yake.c Hivyo, Watswana waliirejezea Biblia kuwa “kinywa cha Yehova.”—Zaburi 83:18.

  • Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Aprili 1
    • c Mwaka wa 1838, Moffat alikamilisha tafsiri ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo. Kwa msaada wa mshiriki fulani, alimaliza kutafsiri Maandiko ya Kiebrania mwaka wa 1857.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki