-
Walilipenda Neno la MunguMnara wa Mlinzi—2009 | Juni 1
-
-
“Ilionekana Kana Kwamba Haiwezekani”
Licha ya upinzani wa familia na marafiki, mmishonari Mwingereza Robert Morrison, aliazimia kabisa kuchapisha Biblia nzima katika Kichina, hivyo akafunga safari kwenda China mwaka wa 1807. Kazi yake ya kutafsiri haikuwa rahisi. Charles Grant, aliyekuwa mkurugenzi wa Kampuni ya East India alisema: “Kazi hiyo ilionekana kana kwamba haiwezekani.”
Alipofika China, Morrison alitambua kwamba Wachina hawakuruhusiwa kuwafundisha wageni lugha yao, na yeyote aliyefanya hivyo aliuawa. Kwa ajili ya usalama wake na wa wale waliokubali kumfundisha Kichina, Morrison hakutoka nje kwa muda. Ripoti fulani inasema kwamba “baada ya kujifunza kwa miaka miwili, Morrison aliweza kusoma, kuandika, na kuzungumza zaidi ya lahaja moja ya lugha ya Mandarin.” Muda si muda, maliki alitoa agizo kukataza uchapishaji wa vitabu vya Kikristo na yeyote aliyevichapisha aliuawa. Licha ya tisho hilo, Morrison alikamilisha Biblia nzima katika lugha ya Kichina mnamo Novemba (Mwezi wa 11) 25, 1819.
Kufikia mwaka wa 1836, nakala karibu 2,000, za Biblia nzima, nakala 10,000 za Maandiko ya Kigiriki, na visehemu mbalimbali 31,000 za Biblia katika Kichina zilikuwa zimechapishwa. Kwa kuwa watu hao walilipenda Neno la Mungu, walifanya kazi “iliyoonekana kana kwamba haiwezekani,” iwezekane.
-
-
Walilipenda Neno la MunguMnara wa Mlinzi—2009 | Juni 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 10]
Robert Morrison na tafsiri yake ya Biblia ya Kichina
[Hisani]
In the custody of the Asian Division of the Library of Congress
Robert Morrison, engraved by W. Holl, from The National Portrait Gallery Volume IV, published c.1820 (litho), Chinnery, George (1774-1852) (after)/Private Collection/Ken Welsh/The Bridgeman Art Library International
-