Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kunaswa Katika Tone la Manjano
    Amkeni!—2002 | Septemba 22
    • Kunaswa Katika Tone la Manjano

      NA MWANDISHI WA AMKENI! KATIKA JAMHURI YA DOMINIKA

      CHUNGU anapanda shina la mti mbiombio pasipo kujua kwamba kuna hatari mbele yake. Kwa ghafula, mguu wake mmoja unakwama, kisha ule mwingine unakwama pia, halafu chungu huyo ananaswa katika utomvu wa mti huo ulio kama asali. Tone jingine linadondoka na kumfunika kabisa. Hawezi kutoroka. Mwishowe, utomvu huo wenye kunata ambao umemfunika chungu unaanguka chini. Chungu huyo aliyenaswa anapelekwa na maji ya mvua hadi mtoni, ambako anafunikwa na matope. Maelfu ya miaka baadaye, chungu huyo anapatikana tena akiwa amehifadhiwa vizuri katika lile tone la manjano. Utomvu huo umekauka na kuwa kaharabu—mojawapo ya vito vyenye thamani zaidi.

      Ni mambo gani yanayojulikana kuhusu kaharabu? Je, tunaweza kujua mambo ya kale kwa kuchunguza kaharabu na wadudu waliomo ndani yake? Je, vitu hivyo vinaweza kusaidia kurudisha viumbe waliotokomea zamani?

  • Kunaswa Katika Tone la Manjano
    Amkeni!—2002 | Septemba 22
    • Kaharabu hutengenezwaje? Kwanza, ganda la mti hupasuka tawi linapovunjika, shina linapokatwa, au mti huo unapovamiwa na mbawakavu wanaoharibu miti. Kisha utomvu wenye kunata hutiririka ili kuziba shimo hilo. Wadudu au viumbe wengine wadogo hunaswa na hatimaye hufunikwa kabisa na utomvu huo. Kwa kawaida utomvu wa mti huwa na maji na virutubisho, lakini utomvu huo wenye kunata una michanganyiko ya kemikali za tapeni, alkoholi, na esta. Kemikali hizo hukausha na kuua wadudu walionaswa na hata mimea. Kunapokuwa na mazingira yanayofaa, utomvu huo hukauka polepole na kufanyiza kaharabu, kisha huhifadhi vitu vilivyonaswa kwa maelfu ya miaka. Kwa hiyo, kaharabu ni utomvu wenye kunata wa miti ya kale.

  • Kunaswa Katika Tone la Manjano
    Amkeni!—2002 | Septemba 22
    • Anataka kuona vitu vilivyonaswa ndani—iwe ni wanyama wa kale, wadudu, au viumbe wengine ambao huenda wakawa wamenaswa katika kaharabu hiyo. Kati ya vipande 100 vya kaharabu ya Dominika, unaweza kumwona mdudu 1. Kwa upande mwingine, unaweza kumwona mdudu 1 tu kati ya vipande 1,000 vya kaharabu ya Baltiki.

  • Kunaswa Katika Tone la Manjano
    Amkeni!—2002 | Septemba 22
    • Kuona Msitu wa Kale Akilini

      Kwa sababu ya sifa zake za kipekee, kaharabu na vitu vilivyonaswa ndani yake vimedumu kwa muda mrefu kuliko miti iliyotokeza kaharabu yenyewe. Viumbe na mimea mingi ya kale imegeuka kuwa miamba na madini, lakini sivyo ilivyo na wanyama na mimea walionaswa katika kaharabu. Iwapo kaharabu inaweza kuonekana ndani, viumbe walionaswa ndani wanaweza kuchunguzwa na kupigwa picha bila kuwaharibu. Hivyo, kuchunguza kaharabu ni njia bora ya kufahamu vitu vya kale kwa sababu ina habari kuhusu wadudu, wanyama wadogo, mimea, na jinsi hali ya hewa ilivyokuwa zamani sana.

      Ni viumbe gani wenye thamani zaidi ambao wamepatikana katika kaharabu? Inategemea maoni ya mkusanyaji wa kaharabu. Wapenzi wa kaharabu wanasema kwamba nge, mijusi, na vyura ndio viumbe watatu wenye thamani zaidi ambao wanapatikana katika kaharabu. Kwa kuwa wao ni wakubwa na wenye nguvu kuliko wadudu wengi, wengi wao wangeweza kujinasua kwa urahisi kutoka kwenye utomvu. Kwa kawaida wale walionaswa walikuwa wadogo sana au labda walidhoofishwa na ugonjwa au kujeruhiwa na wanyama wenye kuwinda. Je, ni rahisi kupata viumbe hao watatu katika kaharabu? Si rahisi hata kidogo! Mkusanyaji mmoja anakadiria kwamba ni nge 30 hadi 40 tu, mijusi 10 hadi 20 tu, na vyura 9 ambao wamewahi kupatikana. Wale wanaopatikana wana thamani kubwa sana. Kipande kimoja cha kaharabu chenye chura mdogo kilipatikana mwaka wa 1997 na kina thamani ya zaidi ya dola 50,000 za Marekani.

      Wanasayansi fulani husisimuliwa na vitu vingine vilivyonaswa. Kwa kuwa mara nyingi wadudu walinaswa kwa ghafula, vipande vingi vya kaharabu vina habari za kale. Inawezekana kupata habari kuhusu tabia za wadudu, kama vile wadudu wenye kuwinda na wale waliowindwa. Vipande fulani vilivyo na mayai, viluwiluwi, mayai ya buibui, au buibui wachanga huwawezesha wanasayansi kuchunguza hatua za ukuzi wa wadudu. Kipande kimoja cha kaharabu, kinachohifadhiwa katika jumba la makumbusho huko Stuttgart, Ujerumani, kina kikundi cha chungu 2,000.

      Vivyo hivyo, habari kuhusu mimea ya misitu ya kale inaweza kupatikana kwa kuchunguza vitu vilivyonaswa ndani ya kaharabu. Inawezekana kutambua mimea na miti mingi ya kale kwa kuchunguza maua, viyoga, kuvumwani, majani, na mbegu zilizohifadhiwa katika kaharabu. Isitoshe, wanasayansi wana uhakika kwamba mitini ilikuwepo, hata ingawa hawajawahi kamwe kupata majani wala matawi yake. Kwa nini? Kwa sababu aina kadhaa za nyigu zimepatikana katika kaharabu—nyigu ambao huishi tu katika mitini. Kwa hiyo, ni jambo la akili kukata kauli kwamba mitini ilikuwepo msituni.

      Kurudisha Viumbe Waliotokomea?

      Miaka kadhaa iliyopita filamu moja ilionyesha kwamba wanyama wakubwa sana wa kale wangeweza kufanyizwa tena kwa kutumia DNA ya damu yao ambayo ilipatikana katika mbu waliokuwa ndani ya kaharabu. Wanasayansi wengi wanasema kwamba hilo haliwezekani. Viumbe wote wana chembe zinazoitwa DNA zinazoamua tabia wanazorithi. Kupitia majaribio ya kisayansi, sehemu ndogo za DNA zimepatikana katika wadudu na mimea kadhaa iliyo ndani ya kaharabu. Hata hivyo, majaribio hayo hayawezi kutokeza tena viumbe waliotokomea.

      DNA hiyo imeharibika na pia si kamili. Kulingana na kadirio moja, huenda habari zilizopatikana katika sehemu hizo za DNA hazizidi sehemu moja ya milioni moja ya habari zote zilizo katika msimbo wa chembe za urithi za kiumbe huyo. Yasemekana kwamba kukusanya habari zote hizo kuhusu msimbo wa viumbe hao ni kama kujaribu kuunda tena kitabu chenye maelfu ya kurasa kutoka kwa sentensi moja isiyoeleweka na isiyo kamili.a

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki