Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye Tamati
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Hasira-Kisasi ya Yehova Dhidi ya “Dunia”

      2. Hutokea nini malaika wa kwanza anapomimina bakuli lake katika dunia, na ni nini kinachofananishwa na dunia?

      2 Malaika wa kwanza aanza kutenda! “Na wa kwanza akaenda zake na akamimina bakuli lake ndani ya dunia. Na donda lenye kuumiza na lenye kudhuru likaja kuwa juu ya watu ambao walikuwa na alama ya hayawani-mwitu na ambao walikuwa wakiabudu mfano wake.” (Ufunuo 16:2, NW) Kama katika kile kisa cha ule mpigo wa kwanza wa tarumbeta, hapa “dunia” hufananisha ule mfumo wa kisiasa ambao huonekana kuwa imara ambao Shetani alianza kujenga hapa duniani huko nyuma katika wakati wa Nimrodi, miaka zaidi ya 4,000 iliyopita.—Ufunuo 8:7, NW.

      3. (a) Serikali nyingi zimedaije kile kinachokuwa sawa na ibada kutoka kwa raia zao? (b) Mataifa yametokeza nini kuwa kibadala cha Ufalme wa Mungu, na tokeo ni nini kwa wale wanaokiabudu?

      3 Katika hizi siku za mwisho, serikali nyingi zimedai kile ambacho kimekuwa kama ibada kutoka kwa raia wazo, zikisisitiza kwamba lazima Serikali itukuzwe juu ya Mungu au ushikamanifu mwingine wowote. (2 Timotheo 3:1; linga Luka 20:25; Yohana 19:15.) Tangu 1914 imekuwa kawaida kwa mataifa kuandikisha vijana wao jeshini kwa nguvu ili kupiga vita, au kuwa tayari kupiga vita, aina ya vita ya ujumla ambayo imetia sana kurasa za historia ya ki-siku-hizi madoa ya damu. Wakati wa siku ya Bwana mataifa yametokeza pia, kuwa kibadala cha Ufalme wa Mungu, mfano wa hayawani—Ushirika wa Mataifa na mwandamizi wao, Umoja wa Mataifa. Ni kufuru kama nini kupiga mbiu, kama vile wamefanya mapapa wa hivi karibuni, kwamba baraza hili lililofanywa na mwanadamu ndilo tumaini pekee la mataifa kwa amani! Hupinga kwa uthabiti Ufalme wa Mungu. Wale wanaoliabudu wanakuwa wachafu kiroho, wenye vidonda, kama vile Wamisri waliopinga Yehova katika siku ya Musa walipigwa kwa tauni ya vidonda na majipu halisi.—Kutoka 9:10, 11.

      4. (a) Yaliyomo katika bakuli la kwanza la kasirani ya Mungu yanakazia nini kwa uthabiti? (b) Yehova huwaonaje wale wanaokubali alama ya hayawani-mwitu?

      4 Yaliyomo katika bakuli hili hukazia kwa uthabiti uchaguzi ulio mbele ya wanadamu: Ni lazima wapatwe na ama kutoidhiniwa na ulimwengu ama ghadhabu ya Yehova. Aina ya binadamu imeshurutishwa kukubali alama ya hayawani-mwitu, kwa kusudi la kwamba “yeyote asipate kuweza kununua au kuuza isipokuwa mtu aliye na alama, jina la hayawani-mwitu au nambari ya jina lake.” (Ufunuo 13:16, 17, NW) Lakini kuna hasara katika hili! Yehova huwaona wale wanaokubali hiyo alama kuwa wakipigwa na “donda lenye kuumiza na lenye kudhuru.” Tangu 1919 wao wametiwa alama peupe kuwa wamekataa Mungu aliye hai. Mipango yao ya kisiasa haina fanikio, nao hupatwa na maumivu makali. Kiroho, wao ni wachafu. Wasipotubu, ugonjwa huu “wenye kuumiza” utaleta kifo, kwa kuwa hii ni siku ya Yehova ya hukumu. Hakuna uwanja wa kutokuwamo kati ya kuwa sehemu ya huu mfumo wa mambo wa ulimwengu na kutumikia Yehova upande wa Kristo wake.—Luka 11:23; linga Yakobo 4:4.

  • Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye Tamati
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Picha katika ukurasa wa 221]

      “Ndani ya Dunia”

      Jamii ya Yohana imetangaza wazi hasira-kisasi ya Yehova dhidi ya “dunia” kwa taarifa kama zifuatazo:

      “Baada ya karne nyingi za jitihada, vyama vya kisiasa vimejithibitisha kutoweza kwavyo kukabiliana na hali za wakati uliopo na kutatua matatizo yenye kutaabisha. Watalaamu wa uchumi na wakuu wa serikali, wakichunguza swali hilo kwa bidii-endelevu, wanapata kwamba hawawezi kufanya kitu.”—Millions Now Living Will Never Die, 1920, ukurasa 61.

      “Hakuna serikali hata moja duniani leo inayotosheleza kisehemu cha ulimwengu kwa kadiri yoyote yenye kuridhisha. Mengi ya mataifa yanatawalwa na madikteta. Ulimwengu kwa ujumla karibu umefilisika.”—A Desirable Government, 1924, ukurasa 5.

      “Kukomesha taratibu ya mambo haya . . . ndiyo njia peke yake ya kuondoa uovu katika dunia na kuipa nafasi amani na haki kusitawi.”—“Habari Njema Hizi za Ufalme,” ukurasa 25.

      “Mpango uliopo sasa wa ulimwengu umejionyesha wazi namna ulivyo kwa kuzidi kutenda dhambi nyingi, mabaya na uasi juu ya Mungu na mapenzi yake. . . . Hauwezi kubadilishwa uwe mzuri. Kwa hiyo, lazima upotelee mbali!”—Mnara wa Mlinzi, Juni 15, 1982, ukurasa 6.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki