-
Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye TamatiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Bahari Yawa Damu
5. (a) Hutukia nini wakati lile bakuli la pili linapomiminwa? (b) Yehova anawaonaje wale wanaokaa katika ile bahari ya mfano?
5 Bakuli la pili la kasirani ya Mungu lazima sasa limiminwe. Itamaanisha nini kwa aina ya binadamu? Yohana atuambia: “Na wa pili akamimina bakuli lake ndani ya bahari. Na hiyo ikawa damu kama ya binadamu mfu, na kila nafsi hai ikafa, ndiyo, vitu vilivyo katika bahari.” (Ufunuo 16:3, NW) Kama mpigo wa pili wa tarumbeta, bakuli hili linaelekezwa dhidi ya “bahari”—tungamo la binadamu lenye kuvurugika, lenye kuasi, lililotenganishwa na Yehova. (Isaya 57:20, 21; Ufunuo 8:8, 9, NW) Machoni pa Yehova, “bahari” hii ni kama damu, isiyowafaa viumbe kuishi ndani yayo. Ndiyo sababu Wakristo lazima wawe si sehemu ya ulimwengu. (Yohana 17:14, NW) Kumiminwa kwa bakuli la pili la kasirani ya Mungu hufunua kwamba aina ya binadamu yote inayokaa katika bahari hii imekufa machoni pa Yehova. Kwa sababu ya daraka la jumuiya, aina ya binadamu ina hatia kubwa ya umwagaji-damu isiyo na hatia. Siku ya kasirani ya Yehova iwasilipo, wao watakufa kihalisi mikononi mwa majeshi yake ya kufisha.—Ufunuo 19:17, 18; linga Waefeso 2:1; Wakolosai 2:13.
-
-
Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye TamatiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Picha katika ukurasa wa 223]
“Ndani ya Bahari”
Zifuatazo ni chache tu za taarifa zilizochapishwa kwa muda wa miaka iliyopita na jamii ya Yohana zikipiga mbiu ya hasira-kisasi ya Mungu dhidi ya “bahari” isiyotulia, yenye uasi ya aina ya binadamu isiyohofu Mungu iliyotenganishwa na Yehova:
“Historia ya kila taifa huonyesha kwamba imekuwa ni mng’ang’ano kati ya matabaka. Imekuwa ni wachache dhidi ya wengi. . . . Ming’ang’ano hii imetokeza mapinduzi makubwa mengi, kuteseka kwingi na umwagaji-damu mwingi.”—Government, 1928, ukurasa 244.
Katika ulimwengu mpya, “‘bahari’ ya mfano ya watu wasiotulia, wenye kuasi, wasiohofu Mungu ambao kutoka kwao hayawani-mwitu alipanda muda mrefu uliopita atumiwe na Ibilisi itakuwa imeenda.”—The Watchtower, Septemba 15, 1967, ukurasa 567.
“Jamii ya sasa ya kibinadamu ni yenye ugonjwa kiroho. Hakuna mmoja wa sisi awezaye kuiokoa, kwa maana Neno la Mungu laonyesha kwamba ugonjwa wayo unaongoza kwenye mauti yake.”—Amani ya Kweli na Usalama wa Kweli—Kutoka Chanzo Gani?, 1974, ukurasa 131.
-