Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye Tamati
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Kiti cha Ufalme cha Hayawani-Mwitu

      15. (a) Bakuli la tano lamiminwa juu ya nini? (b) Ni nini kilicho “kiti cha ufalme cha hayawani-mwitu,” na ni nini kinachohusika katika kumiminwa kwa bakuli juu yacho?

      15 Malaika anayefuata anamimina bakuli lake juu ya nini? “Na wa tano akamimina bakuli lake juu ya kiti cha ufalme cha hayawani-mwitu.” (Ufunuo 16:10a, NW) “Hayawani-mwitu” ni mfumo wa kiserikali wa Shetani. Hauna kiti cha ufalme halisi, kama vile hayawani-mwitu asivyo halisi. Hata hivyo, mtajo wa kiti cha ufalme, huonyesha kwamba huyo hayawani-mwitu ametumia mamlaka ya kifalme juu ya aina ya binadamu; hii inapatana na uhakika wa kwamba kila moja ya pembe za hayawani-mwitu ina taji la kifalme. Kwa kweli, hicho “kiti cha ufalme cha hayawani-mwitu” ndicho msingi, au chimbuko, la mamlaka hiyo.b Biblia hufunua hali ya kweli ya mamlaka ya kifalme ya huyo hayawani-mwitu wakati inaposema kwamba “drakoni akampa hayawani nguvu zake na kiti cha ufalme chake na mamlaka kubwa.” (Ufunuo 13:1, 2; 1 Yohana 5:19, NW) Hivyo, kumiminwa kwa bakuli juu ya kiti cha ufalme cha hayawani-mwitu kunahusu mbiu yenye kufunua daraka la kweli ambalo Shetani amekuwa nalo na ambalo angali nalo katika kuunga mkono na kuendeleza huyo hayawani-mwitu.

      16. (a) Mataifa yanatumikia nani, yawe yanajua hivyo au hayajui? Fafanua. (b) Ulimwengu huonyeshaje utu wa Shetani? (c) Kiti cha ufalme cha hayawani-mwitu kitapinduliwa lini?

      16 Uhusiano huu kati ya Shetani na mataifa unadumishwaje? Shetani alipomshawishi Yesu, yeye alimwonyesha falme zote za ulimwengu katika njozi na akamtolea “mamlaka yote hii na utukufu wazo.” Lakini lilikuwako sharti moja—kwanza Yesu alipaswa afanye tendo la ibada mbele ya Shetani. (Luka 4:5-7, NW) Je! sisi tunaweza kudhani kwamba serikali za ulimwengu zinapokea mamlaka yazo kwa bei ndogo zaidi ya hiyo? Hasha. Kulingana na Biblia, Shetani ndiye kamungu ka huu mfumo wa mambo, hivi kwamba, yawe mataifa yanajua au hayajui, yanatumikia yeye. (2 Wakorintho 4:3, 4, NW)c Hali hii inafunuliwa na muundo wa mfumo wa ulimwengu uliopo, ambao umejengwa juu ya utukuzaji taifa wa kijinga, chuki, na kujipendeza kibinafsi. Umeundwa kitengenezo namna Shetani anavyotaka—kufuliza kutunza aina ya binadamu chini ya udhibiti wake. Ufisadi katika serikali, pupa ya kutaka mamlaka, ubalozi wa uwongo-uwongo, shindano la kuunda silaha—hayo huonyesha utu wa Shetani uliotwezwa. Ulimwengu unachangia viwango vya Shetani vyenye utovu wa uadilifu, hivyo kumfanya yeye kuwa kamungu kao. Kiti cha ufalme cha hayawani-mwitu kitapinduliwa wakati huyo hayawani apatwapo na mzimiko na mwishowe Mbegu ya mwanamke wa Mungu imtiapo Shetani mwenyewe ndani ya abiso.—Mwanzo 3:15; Ufunuo 19:20, 21; 20:1-3, NW.

      Giza na Umivu Lenye Kugugunya

      17. (a) Kumiminwa kwa bakuli la tano huhusianaje na giza la kiroho ambalo sikuzote limefunika ufalme wa hayawani-mwitu? (b) Watu wanatendaje kwa kuitikia kumiminwa kwa bakuli la tano la kasirani ya Mungu?

      17 Ufalme wa hayawani-mwitu huyu umekuwa katika giza la kiroho tangu ulipoanza. (Linga Mathayo 8:12; Waefeso 6:11, 12.) Bakuli la tano linaleta tangazo la peupe lenye mkazo mkubwa juu ya giza hili. Hata linalifanyia drama, kwa kuwa bakuli hili la kasirani ya Mungu humiminwa juu ya kiti cha ufalme chenyewe cha hayawani-mwitu wa ufananisho. “Na ufalme wake ukatiwa giza, na wao wakaanza kugugunya ndimi zao kwa ajili ya maumivu yao, lakini wao wakamkufuru Mungu wa mbingu kwa ajili ya maumivu yao na kwa ajili ya vidonda vyao, na wao hawakutubu kazi zao.”—Ufunuo 16:10b, 11, NW.

      18. Kuna ulingano gani kati ya mpigo wa tano wa tarumbeta na bakuli la tano la kasirani ya Mungu?

      18 Mpigo wa tano wa tarumbeta si sawa kabisa na bakuli la tano la kasirani ya Mungu, kwa kuwa mpigo wa tarumbeta ulitangaza tauni ya nzige. Lakini angalia kwamba wakati wa kuachiliwa tauni hiyo ya nzige, kulikuwako na kutiwa giza kwa jua na hewa. (Ufunuo 9:2-5) Na kwenye Kutoka 10:14, 15 (NW), tunasoma hivi kuhusu wale nzige ambao kwa hao Yehova alipiga Misri: “Walikuwa wenye kulemea sana. Kabla ya wao kulikuwa hakujatokea kamwe nzige kama wao, na hakutatokea kamwe wengine katika njia hii baada yao. Na wao wakaenda wakifunika uso wote wenye kuonekana wa bara zima, na bara likapata kuwa giza ti.” Ndiyo, giza ti! Leo, giza la kiroho la ulimwengu limekuwa wazi sana likiwa tokeo la kuvumishwa kwa tarumbeta ya tano na kumiminwa kwa bakuli la tano la kasirani ya Mungu. Ujumbe wenye kuchoma kwa uchungu ambao umepigiwa mbiu na bumba la nzige wa ki-siku-hizi huleta mateso na maumivu kwa wale waovu ambao “wamependa giza badala ya nuru.”—Yohana 3:19, NW.

      19. Kupatana na Ufunuo 16:10, 11, kufichuliwa peupe kwa Shetani kuwa mungu wa huu mfumo wa mambo kunasababisha nini?

      19 Akiwa mtawala wa ulimwengu, Shetani amesababisha utofurahifu mwingi na mateso. Njaa kuu, vita, jeuri, uhalifu, matumizi mabaya ya dawa za kulevya, utovu wa adili, magonjwa yenye kupitishwa kingono, utovu wa haki, unafiki wa kidini—haya na zaidi ni alama za mfumo wa mambo wa Shetani. (Linga Wagalatia 5:19-21.) Hata hivyo, ufichulio wa peupe wa Shetani kuwa ndiye mungu wa huu mfumo wa mambo ulisababisha maumivu na tahayari kwa wale ambao huishi kwa viwango vyake. “Wao wakaanza kugugunya ndimi zao kwa ajili ya maumivu yao,” hasa katika Jumuiya ya Wakristo. Wengi huona uchungu moyoni kwa vile ukweli hufunua mtindo wao wa maisha. Baadhi yao huuona kuwa tisho, nao hunyanyasa wale wanaoutangaza. Wanakataa Ufalme wa Mungu na kutusi jina takatifu la Yehova. Hali yao ya kidini yenye ugonjwa na yenye madonda madonda inafunuliwa wazi, hivi kwamba wao wanakufuru Mungu wa mbingu. La, wao ‘hawatubu kazi zao.’ Kwa hiyo sisi hatuwezi kutazamia kuongolewa kwa tungamo la watu kabla ya mwisho wa huu mfumo wa mambo.—Isaya 32:6.

  • Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye Tamati
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Picha katika ukurasa wa 227]

      “Juu ya Kiti cha Ufalme cha Hayawani-Mwitu”

      Mashahidi wa Yehova wamefichua kiti cha ufalme cha hayawani-mwitu na wakatangaza wazi shutumu la Yehova juu yacho kwa taarifa kama hizi:

      “Watawala na waongozi wa kisiasa wa mataifa wanavutwa na kani zisizo za kibinadamu, zenye makusudi mabaya, zinazowaendesha bila kupingwa katika mwendo wa ujiuaji kwenye mpambano wa kukata maneno wa Har–Magedoni.”—After Armageddon—God’s New World, 1953, ukurasa 8.

      “‘Hayawani-Mwitu’ wa serikali za kibinadamu zisizo za kitheokrasi alipata uwezo, mamlaka na kiti cha ufalme chake kutoka kwa Drakoni. Kwa hiyo lazima atii amri ya chama, amri ya Drakoni.”—After Armageddon—God’s New World, 1953, ukurasa 15.

      “Mataifa Yasiyo ya Kiyahudi yanaweza kujikuta yenyewe tu . . . upande wa Hasimu Mkuu wa Mungu, Shetani Ibilisi.”—Azimio lililokubaliwa kwenye “Ushindi wa Kimungu” Mkusanyiko wa Kimataifa, 1973.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki