-
Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye TamatiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Mto Eufrati Wakaushwa
20. Mpigo wa sita wa tarumbeta na pia kumwagwa kwa bakuli la sita huhusishaje ndani mto Eufrati?
20 Mpigo wa sita wa tarumbeta ulitoa habari ya kuachiliwa kwa “malaika wanne ambao wamefungwa kwenye mto mkubwa Eufrati.” (Ufunuo 9:14, NW) Kihistoria, Babuloni lilikuwa jiji kubwa ambalo lilikalia mto Eufrati. Na katika 1919 kuachiliwa kwa malaika wanne wa ufananisho kuliandamana na anguko la maana la Babuloni Mkubwa. (Ufunuo 14:8, NW) Basi, inastahili kuangaliwa kwamba, bakuli la sita la kasirani ya Mungu huhusisha ndani pia mto Eufrati: “Na wa sita akamimina bakuli lake juu ya mto mkubwa Eufrati, na maji yao yakakauka kabisa, ili njia iweze kutayarishwa kwa ajili ya wafalme kutoka zukio la jua.” (Ufunuo 16:12, NW) Hii vilevile ni habari mbaya kwa Babuloni Mkubwa!
21, 22. (a) Maji yenye kinga ya mto Eufrati yalikaukiaje Babuloni katika 539 K.W.K.? (b) Maji ambayo Babuloni Mkubwa anaketia ni nini, na hata sasa maji haya ya ufananisho yanakaukaje?
21 Katika wakati wa upeo wa Babuloni la kale, maji mengi ya Eufrati yalikuwa sehemu kubwa ya mfumo wa kinga yalo. Katika 539 K.W.K. maji hayo yalikaushwa wakati yalipogeuzwa kando kutoka njia yayo na Sairasi kiongozi Mwajemi. Hivyo, njia ikafunguliwa kwa Sairaisi Mwajemi na Dario Mmedi, wafalme kutoka “zukio la jua” (yaani, mashariki), waingie Babuloni na kulishinda. Katika ile saa ya hatari, mto Eufrati ulishindwa kuwa kinga ya hilo jiji kubwa. (Isaya 44:27–45:7; Yeremia 51:36, NW) Jambo fulani kama hilo linakaribia kutukia kwa Babuloni wa ki-siku-hizi, mfumo wa ulimwenguni pote wa dini bandia.
22 Babuloni Mkubwa “huketi juu ya maji mengi.” Kulingana na Ufunuo 17:1, 15, (NW), hayo hufananisha “vikundi vya watu na umati wa watu na mataifa na ndimi”—magenge ya wafuasi ambao yeye huwaona kuwa himaya. Lakini “maji” yanakauka! Katika Ulaya Magharibi, ambako hapo kwanza alikuwa na uvutano mwingi, mamia ya maelfu wamepuuza dini waziwazi. Katika mabara fulani, kwa miaka mingi kulikuwa na sera iliyojulishwa wazi kujaribu kuharibu uvutano wa dini. Matungamo katika mabara hayo hayakuinuka kumsaidia. Hali kadhalika, ujapo wakati wa Babuloni Mkubwa kuharibiwa, hesabu yenye kupungua ya wafuasi wake haitathibitika kuwa himaya kwa vyovyote. (Ufunuo 17:16) Ingawa yeye hudai kuwa na washiriki mamia ya mamilioni, Babuloni Mkubwa atajikuta akiwa bila kinga dhidi ya “wafalme kutoka zukio la jua.”
23. (a) Ni nani waliokuwa wafalme kutoka “zukio la jua” katika 539 K.W.K.? (b) Ni nani walio “wafalme kutoka zukio la jua” wakati wa siku ya Bwana, nao wataharibuje Babuloni Mkubwa?
23 Hawa wafalme ni nani? Katika 539 K.W.K. wao walikuwa Dario Mmedi na Sairasi Mwajemi, ambao walitumiwa na Yehova kushinda jiji la kale la Babuloni. Katika hii siku ya Bwana, dini bandia ya Babuloni Mkubwa itaharibiwa pia na watawala wa kibinadamu. Lakini kwa mara nyingine tena, hii itakuwa hukumu ya kimungu. Yehova Mungu na Yesu Kristo, “wafalme kutoka zukio la jua,” watakuwa wametia katika mioyo ya watawala wa kibinadamu “fikira” wamgeukie Babuloni Mkubwa na kumharibu kabisa. (Ufunuo 17:16, 17, NW) Kumwagwa kwa bakuli la sita hupiga mbiu peupe kwamba hukumu hii inakaribia kutekelezwa!
-
-
Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye TamatiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Picha katika ukurasa wa 229]
“Maji Yao Yakakauka Kabisa”
Hata sasa, uungaji-mkono wa dini ya Kibabuloni unakauka kabisa mahali pengi, kuonyesha jambo litakalotukia wakati “wafalme kutoka zukio la jua” watakapofanya shambulio lao.
“Uchunguzi wa maoni ya watu wa taifa zima ulipata kwamba asilimia 75 ya wale wanaoishi katika maeneo ya manispaa [ya Thailandi] hawaendi hata kidogo kwenye mahekalu ya Kibuddha kusikiliza mahubiri, hali hesabu ya wale wanaozuru mahekalu mashambani inazidi kupungua kufika yapata asilimia hamsini.”—Bangkok Post, Septemba 7, 1987, ukurasa 4.
“Mzungu umekwisha katika Utao katika bara [China] ambako ulianzia zapata mileani mbili zilizopita. . . . Wakiwa bila vidude vya kufanyia mizungu ambavyo kwavyo wao na watangulizi wao walizoea kupata ufuasi mwingi, washiriki wa ukuhani wanajikuta wakiwa bila waandamizi, karibu wakikabili mzimiko wa Utao ukiwa imani iliyopangwa kitengenezo katika bara kuu.”—The Atlanta Journal and Constitution, Septemba 12, 1982, ukurasa 36-A.
“Japani . . . ina mmojapo misongano mikubwa zaidi sana ya wamisionari wa kigeni ulimwenguni, karibu 5,200, hata hivyo . . . punde kuliko asilimia 1 ya idadi ya watu ni Wakristo. . . . Padri mmoja wa Kifransiska anayefanya kazi hapa tangu miaka ya 1950 . . . anaitikadi kwamba ‘siku ya wamisionari wa kigeni katika Japani imekwisha.’”—The Wall Street Journal, Julai 9, 1986, ukurasa 1.
Katika Uingereza wakati wa miongo mitatu iliyopita, “karibu makanisa ya Kianglikana 2,000 kati ya yale 16,000 yamefungwa kwa sababu ya kutotumiwa. Hadhirina imepungua kuwa miongoni mwa zile za chini zaidi sana za nchi zinazokiri kuwa za Kikristo. . . . ‘Sasa hali ni kwamba Uingereza si nchi ya Kikristo,’ akasema [Askofu wa Durham].”—The New York Times, Mei 11, 1987, ukurasa A4.
“Baada ya saa nyingi za majadiliano makali, Bunge [la Ugiriki] liliidhinisha leo sheria itungwe, ikiiwezesha Serikali ya Kisoshalisti itwae mali zenye mashamba makubwa mno zinazoshikiliwa na Kanisa Orthodoksi la Ugiriki . . . Zaidi ya hilo, sheria hiyo inawapa wasio viongozi wa kanisa udhibiti wa mabaraza ya kanisa na halmashauri zenye madaraka ya kusimamia vitega-uchumi vya kanisa vyenye thamani kubwa kutia ndani mahoteli, mashimo ya kuchimba marumaru na majengo ya maofisi.”—The New York Times, Aprili 4, 1987, ukurasa 3.
-