-
Ubongo Wako Unatatanisha AjabuAmkeni!—1999 | Mei 8
-
-
Kuchunguza Ubongo Wako
Mikunjokunjo ya utando wa bongo kubwa au utando wa nje wa ubongo, ndiyo inayotokeza zaidi. (Ona mchoro ulio kwenye ukurasa wa 4 na sanduku kwenye ukurasa wa 8.) Utando huo uliokunjamana na wenye unene wa milimeta kadhaa na ambao una rangi ya kijivu na waridi una asilimia 75 hivi za chembe zote za neva za ubongo ambazo ni kati ya bilioni 10 hadi bilioni 100. Lakini wanasayansi fulani wanasema kwamba hata chembe hizo zote za neva hazisababishi ule utata wa ubongo.
-
-
Ubongo Wako Unatatanisha AjabuAmkeni!—1999 | Mei 8
-
-
Sababu Inayofanya Tusihitaji Kichwa Kikubwa Zaidi
“Kama utando wa bongo kubwa haungekuwa na mikunjokunjo, ubongo ungekaribia kutoshana na mpira wa mchezo wa vikapu, badala ya kutoshana na ngumi mbili zilizokunjwa pamoja.”—Profesa Susan A. Greenfield
-