Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ubongo Wako Hufanyaje Kazi?
    Amkeni!—1999 | Mei 8
    • Ni Nini Hufanyiza Kumbukumbu?

      Kumbukumbu—“labda kitu chenye kustaajabisha zaidi katika uumbaji ulimwenguni pote,” kulingana na Profesa Richard F. Thompson—lahusisha utendaji mbalimbali ulio tofauti wa ubongo. Wachunguzi wengi wa ubongo husema kuna aina mbili za kumbukumbu, za mambo ya hakika na za utaratibu. Kumbukumbu za utaratibu huhusisha stadi na tabia. Kwa upande mwingine, kumbukumbu za mambo ya hakika huhifadhi habari. Kitabu The Brain—A Neuroscience Primer huainisha kumbukumbu kulingana na muda zinazochukua: kumbukumbu fupi sana, ambayo huchukua nukta 10 za sekunde; kumbukumbu fupi, ambayo huchukua sekunde chache; kumbukumbu inayotumika, ambayo huhifadhi mambo yaliyotokea karibuni; kumbukumbu ya muda mrefu, ambayo huweka maneno ambayo yamekaririwa tena na tena na vilevile kuweka stadi za miendo ambayo imefanywa kwa kurudiwa-rudiwa.

      Jambo moja ambalo limefafanuliwa kuhusu kumbukumbu ya muda mrefu ni kwamba utendaji wake huanzia sehemu ya mbele ya ubongo. Habari inayochaguliwa iwe kumbukumbu ya muda mrefu hupita ikiwa ishara ya umeme kwenye sehemu ya ubongo inayoitwa hippocampus. Hapo utaratibu unaoitwa uimarishaji wa muda mrefu huwezesha chembe za neva kupitisha ujumbe.—Ona sanduku “Kuziba Pengo.”

      Nadharia tofauti juu ya kumbukumbu yatokana na wazo la kwamba mawimbi ya ubongo yanatimiza fungu kubwa. Watetezi wa nadharia hiyo wanaamini kwamba mizunguko ya kawaida ya utendaji wa umeme katika ubongo, unaofanana na mapigo ya ngoma, husaidia kushikanisha kumbukumbu pamoja na kudhibiti pindi ambapo chembe tofauti za ubongo zinachochewa.

      Watafiti huamini kwamba ubongo huhifadhi aina mbalimbali za kumbukumbu kwenye sehemu tofauti-tofauti, kila aina ya kumbukumbu ikiunganishwa na eneo la ubongo lenye uwezo wa kuifahamu. Kwa hakika, sehemu fulani za ubongo huchangia kuwako kwa kumbukumbu. Sehemu inayoitwa amygdala, ambayo ni tita la neva linalotoshana na lozi lililo karibu na msingi wa ubongo, hushughulikia kumbukumbu ya hofu. Eneo linaloitwa basal ganglia, hukazia tabia na stadi za mtu, na ubongo wa kisogoni, ambao upo penye msingi wa ubongo, hudhibiti kujifunza miendo na maitikio ya mwili. Inasemekana kwamba ni hapo ndipo tunahifadhi stadi za usawaziko—kwa mfano, usawaziko tunaohitaji ili kuendesha baiskeli.

  • Ubongo Wako Hufanyaje Kazi?
    Amkeni!—1999 | Mei 8
    • Hali fulani inayoitwa uimarishaji wa muda mrefu hutukia wakati ambapo chembe za neva huchochewa kwa ukawaida na kuachilia vipitisha-habari vivuke sinapsi. Watafiti fulani wanaamini kwamba jambo hilo huzivuta chembe za neva pamoja. Wengine hudai kuna uthibitisho kwamba ujumbe hurudi kutoka kwenye chembe ya neva inayoupokea hadi kwenye chembe ya neva inayoupeleka. Jambo hilo husababisha mabadiliko ya kemikali ambayo hutokeza protini zaidi ambazo hutumika kama vipitisha-habari. Basi hivyo vipitisha-habari navyo huimarisha kifungo kilichoko kati ya chembe za neva.

      Kubadilika-badilika kwa miunganisho ya ubongo na uwezo wake wa kunyumbulika, kumetokeza usemi usemao, “Uutumie au Uupoteze.” Basi ili uweze kukumbuka kitu, inafaa ukikariri mara nyingi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki