Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutunza Mali za Bwana-Mkubwa
    Huduma ya Ufalme—1998 | Juni
    • 8 Hata iwe uchapaji uliongezeka kadiri gani Marekani, haukuwa mwingi vya kutosha kugawia ulimwengu wote. Kwa hiyo, miaka iliyofuata vita, utendaji wa uchapaji ulianzishwa au ulikuwa tayari ukiendelea katika nchi nyingi, kutia ndani Afrika Kusini, Denmark, Kanada, Ugiriki, Uingereza, Ujerumani Magharibi, na Uswisi. Kufikia miaka ya mapema ya 1970, Australia, Brazili, Finland, Ghana, Japani, Nigeria, na Filipino zilikuwa zimeongezwa kwenye orodha hiyo. Baadhi ya nchi hizi pia zilitokeza mabuku yaliyojalidiwa. Pia miaka ya mapema ya 1970, wamishonari wa Gileadi walifundishwa stadi za uchapaji na kutumwa katika baadhi ya nchi hizi ili kusaidia ndugu wa huko kazi ya uchapaji.

      9 Miaka ya 1980, idadi ya nchi ambamo magazeti yalikuwa yakichapwa ilifikia kilele cha 51.a

  • Kutunza Mali za Bwana-Mkubwa
    Huduma ya Ufalme—1998 | Juni
    • Mahitaji Mbalimbali ya Kitengenezo

      12 Mifumo hii mipya ilibadilisha mahitaji ya kitengenezo ulimwenguni pote ya utendaji wa kuchapa wa Mashahidi wa Yehova. Matbaa za web hufanya kazi haraka sana kuliko matbaa ya kuchapa kama kwa kupiga muhuri, lakini pia ni ghali sana. Mifumo ya kompyuta inayofanya kazi inayohusiana kama vile, uandishi, utafsiri, uchoraji, na upangaji wa chapa, huku ikiwa na uwezo mwingi kuliko ile mifumo ya zamani, ni ghali sana. Upesi ilionekana kwamba halikuwa jambo la kupunguza gharama kuchapa magazeti katika nchi 51 tofauti-tofauti. Kwa sababu hiyo, katika miaka ya 1990 “msimamizi-nyumba mwaminifu” alichunguza mambo tena. Uamuzi ulikuwa nini?

      13 Uchunguzi ulionyesha kwamba ‘vitu vyenye thamani’ vilivyochangwa na Mashahidi wa Yehova na rafiki zao vingetumiwa vema zaidi kama kazi ya uchapaji ingeunganishwa. Kwa hiyo idadi ya ofisi za tawi zenye kuchapa ilipunguzwa. Ujerumani imechukua uchapaji wa magazeti na fasihi za nchi nyingi za Ulaya Mashariki na Magharibi, kutia ndani nchi kadhaa ambazo zimekuwa zikifanya uchapaji wao wenyewe. Italia huandaa magazeti na fasihi kwa ajili ya sehemu za Afrika na kusini-mashariki mwa Ulaya, kutia ndani Ugiriki na Albania. Katika Afrika, uchapaji wa magazeti hufanywa Nigeria na Afrika Kusini tu. Kuunganishwa hukohuko kulitokea ulimwenguni pote.

      Mambo Fulani ya Kufikiria kwa Uangalifu

      14 Kufikia Julai 1998, uchapaji wa magazeti utakomeshwa katika nchi kadhaa za Ulaya kutia na Austria, Denmark, Ufaransa, Ugiriki, Uholanzi, na Uswisi. Kazi ya uchapaji katika Ulaya itashughulikiwa na Finland, Hispania, Italia, Sweden, Uingereza, na Ujerumani. Katika njia hii, gharama zisizo za lazima zingeepukwa na michango ingetumiwa kwa njia bora kwa ajili ya kazi ya ulimwenguni pote. Iliamuliwaje kwamba nchi kadhaa ziendelee kuwa sehemu za uchapaji na zipi ziache uchapaji? Kupatana na amri yake ya kutunza kwa hekima mali za Bwana-Mkubwa, “msimamizi-nyumba mwaminifu” alikadiria busara ya kuchapa katika kila sehemu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki