Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kansa ya Matiti Utazamie Nini? Ukabiliane Jinsi Gani?
    Amkeni!—2011 | Agosti
    • Ili kuchunguza ikiwa uvimbe wa Conchita ulikuwa na kansa, daktari wake alitumia sindano nyembamba kutoa tishu kutoka kwenye uvimbe huo. Uvimbe huo ulikuwa na kansa. Hivyo, alifanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe huo na tishu zilizozunguka titi. Upasuaji huo ulisaidia pia kuonyesha uvimbe huo ulikuwa umefikia hatua gani (ukubwa, aina, na kuenea kwake) na kuchunguza ulikuwa ukikua upesi kwa kadiri gani.

      Baada ya upasuaji, wagonjwa wengi hupata matibabu mengine ambayo yatazuia kansa isirudi au kuenea. Chembe zenye kansa zinaweza kutoka kwenye uvimbe na kusafiri kupitia mfumo wa damu au mfumo wa limfu, na kuanza kukua tena mahali pengine mwilini. Kuenea kwa kansa hadi kwenye viungo na tishu muhimu kama vile ubongo, ini, uboho wa mfupa, au mapafu ndio hufanya ugonjwa huo uwe hatari.

      Conchita alitibiwa kwa miale na kemikali ili kuharibu chembe za kansa kwenye titi na pia katika sehemu nyingine za mwili. Kwa kuwa uvimbe wenye kansa aliokuwa nao ulichochewa hasa na homoni ya estrojeni, alipewa matibabu ya kuzuia kutokezwa kwa homoni hiyo ili kuzuia uvimbe mpya wenye kansa usitokee.

      Kwa sababu ya maendeleo katika matibabu ya kansa ya matiti, kumekuwa na matibabu mbalimbali ikitegemea umri, afya, historia ya kansa katika familia, na aina ya kansa. Kwa mfano, katika kisa cha mwanamke anayeitwa Arlette, uchunguzi ulifanya kansa yake igunduliwe kabla haijaenea nje ya vijia vya kupitishia maziwa. Kwa hiyo, alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe huo, na titi lake halikukatwa. Kabla ya kufanyiwa upasuaji, Alice alitibiwa kwa kemikali ili kupunguza ukubwa wa uvimbe. Daktari wa Janice aliondoa tu uvimbe na tezi za limfu zilizokuwa karibu, ambazo huwa za kwanza kuingia umajimaji kutoka kwenye uvimbe. Kwa kuwa tezi nyingine hazikuwa na chembe zenye kansa, hakuziondoa. Hilo lilifanya mkono wa Janice usivimbe kwa sababu ya kufungika kwa mishipa ya limfu, jambo ambalo hutokea wakati tezi nyingi za limfu zinapoondolewa.

  • Kansa ya Matiti Utazamie Nini? Ukabiliane Jinsi Gani?
    Amkeni!—2011 | Agosti
    • Je, kuna tumaini lolote la kugunduliwa kwa tiba bora ya kansa ya matiti isiyotokeza madhara? Watafiti wanachunguza matibabu ambayo yatahusisha kutumia mfumo wa kinga wa mwili na dawa ambazo zitalenga hasa utendaji wa chembe za urithi na protini ambazo huchochea ukuzi wa kansa. Kwa sasa, teknolojia iliyoboreshwa ya kupiga picha za eksirei inapaswa kuwasaidia madaktari kutibu kwa njia hususa kwa kutumia miale.

      Wanasayansi pia wanajifunza mambo mengine kuhusu kansa kutia ndani: kuelewa ni kwa nini kansa huenea, kudhibiti chembe za kansa ambazo haziharibiwi kupitia matibabu ya kemikali, kuzuia kugawanyika kwa chembe, na kutibu kila uvimbe kwa njia hususa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki