Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Mipango ilifanywa mara hiyo ili Ndugu Brown atoe hotuba katika Jumba la Ukumbusho la Wilberforce. Katika Aprili 19, kulikuwa hudhurio la watu 500 hivi, kutia na walio wengi wa makasisi wa Freetown. Jumapili iliyofuata alitoa hotuba tena. Habari yake ilikuwa ile ambayo C. T. Russell alikuwa ametumia mara nyingi—“Kwenda Helo na Kurudi. Nani Walio Humo?” Hotuba za Ndugu Brown zilitia ndani kwa ukawaida manukuu ya Maandiko yaliyoangaziwa kwa slaidi za taa ili wasikilizaji waweze kuyaona. Alipokuwa akihutubu, alikuwa akisema hivi kwa kurudiarudia: “Si Brown anayesema, bali Biblia yasema.” Kwa sababu ya hilo, yeye akaja kuitwa “Bible Brown.” Na kama tokeo la utoaji wake wa Kimaandiko, wenye kupatana na akili, baadhi ya washiriki mashuhuri wa kanisa waliondoka kanisani na kuanza utumishi wa Yehova.

      Alisafiri sana ili kuanzisha kazi ya Ufalme katika maeneo zaidi. Kwa kusudi hilo, alitoa mihadhara mingi ya Biblia, na kugawanya kiasi kikubwa cha fasihi, naye aliwatia moyo wengine wafanye vivyo hivyo. Kazi yake ya kueneza evanjeli ilimpeleka katika Gold Coast (sasa ni Ghana), Liberia, Gambia, na Nigeria. Kutoka Nigeria wengine walipeleka ujumbe wa Ufalme katika Benin (wakati huo ikijulikana kuwa Dahomey) na Kamerun. Ndugu Brown alijua kwamba umma hawakuwa na staha kwa ile waliyoiita “dini ya mzungu,” hivyo katika Jumba la Ukumbusho la Glover katika Lagos, alitoa hotuba juu ya kushindwa kwa dini ya Jumuiya ya Wakristo. Baada ya mkutano wasikilizaji hao wenye kuchangamka walipata vitabu 3,900 wavisome na kuvishiriki na wengine.

  • Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Picha katika ukurasa wa 434]

      Kotekote katika Afrika Magharibi, “Bible Brown” alishiriki kwa juhudi katika kufunua ibada bandia

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki