-
Jinsi ya Kupunguza GharamaAmkeni!—2010 | Julai
-
-
Kwa kutumia kanuni hiyo, unaweza “kuhesabu gharama” ya kuishi kulingana na mapato yako ikiwa utapanga bajeti. Kwa njia gani? Hebu jaribu kufanya hivi:
Unapopata mshahara wako, tenga pesa hususa katika vikundi tofauti ili kushughulikia gharama za sasa au za wakati ujao. (Ona sanduku kwenye ukurasa wa 8.) Unapopanga gharama zako, unaweza kuona mahali pesa zako zinaenda na unatumia kiasi gani kununua vitu visivyo vya lazima. Kufanya hivyo kutakusaidia kuamua jinsi unavyoweza kupunguza gharama zako.
Ili upange bajeti inayokufaa, jaribu kutumia mapendekezo yafuatayo.
Tumia Busara Unaponunua Vitu
Raúl alipoachishwa kazi, mke wake Bertha, alibadili mbinu yake ya kununua vitu. Anasema, “Niliangalia matangazo yaliyoonyesha mahali ambapo bidhaa zimepunguzwa bei na maduka ya mboga yaliyouza vitu viwili kwa bei ya kimoja.” Zifuatazo ni mbinu nyingine:
● Pika vyakula vinavyopatikana kwa wingi.
● Jipikie chakula badala ya kununua kilichopikwa na kupakiwa.
● Nunua bidhaa za ziada zinapopatikana kwa wingi au kwa bei ya chini.
● Nunua vitu kwa jumla, lakini jihadhari usijaze vitu vinavyoweza kuharibika upesi.
● Punguza gharama kwa kununua mavazi mazuri yaliyotumika.
● Safiri hadi maeneo ambako bei ni za chini, ikiwa hutatumia pesa nyingi kwa ajili ya usafiri.
● Punguza safari za kwenda dukani.a
Andika
Fred anasema, “Tulilazimika kupanga bajeti, kwa hiyo, niliandika gharama ambazo tulihitaji kulipa mara moja na pesa za matumizi ya mwezi mzima.” Mke wake, Adele, anasema hivi: “Nilijua ni pesa ngapi nitakazotumia ninapoenda sokoni. Nyakati nyingine nilipohitaji kununua kitu cha nyumbani au kwa ajili ya watoto, niliitazama bajeti na kujiambia, ‘Sina pesa za kukinunua, kwa hiyo, tutasubiri hadi mwezi ujao.’ Kuandika kulinisaidia sana!”
Fikiria Kabla ya Kununua
Uwe na zoea la kujiuliza: ‘Je, kweli ninahitaji kitu hiki? Je, kweli kile cha zamani kimechakaa, au ninataka tu kitu kipya?’ Ikiwa hutumii kitu fulani kwa ukawaida, je, si afadhali tu kukodi kitu hicho? Au ikiwa unafikiri kwamba utakitumia mara nyingi, je, unaweza kununua kilichotumika?
Ingawa huenda ikaonekana kuwa jambo dogo kufanya mambo yaliyotajwa hapa juu, yanapofanywa yote yanaweza kusaidia sana! Jambo kuu ni, ukiwa na zoea la kuokoa pesa unazotumia kwa ajili ya vitu vidogovidogo, utafanya hivyo pia unaposhughulikia mambo makubwa.
Tafuta Njia za Kupunguza Gharama
Ili uokoe pesa unazotumia kununua vitu visivyo vya lazima, uwe mbunifu. Kwa mfano, Adele anasema hivi: “Tulikuwa na magari mawili lakini tukauza moja na kutumia hilo lingine. Ili tuokoe pesa tulizotumia kununua petroli, tulipanga kufanya shughuli nyingi kwa wakati mmoja. Tulitumia pesa kwa ajili tu ya vitu vya lazima.” Zifuatazo ni njia nyingine zinazoweza kukusaidia kupunguza gharama:
● Kuza mboga zako nyumbani.
● Fuata maagizo ya watengenezaji wa vifaa, ili vidumu kwa muda mrefu.
● Badili mavazi yako mazuri mara tu unapofika nyumbani kwani kufanya hivyo kutayafanya yadumu yakiwa mapya kwa muda mrefu zaidi.
-
-
Jinsi ya Kupunguza GharamaAmkeni!—2010 | Julai
-
-
[Sanduku/Ramani katika ukurasa wa 8]
Jinsi ya Kupanga Bajeti
(1) Andika gharama za lazima za kila mwezi. Weka rekodi ya pesa zote unazotumia mwezi mzima kwa chakula, nyumba, malipo ya huduma mbalimbali, gharama za gari, na kadhalika. Kwa ajili ya gharama zinazolipiwa kila mwaka, gawa gharama hizo mara 12 ili uhifadhi pesa hizo kila mwezi.
(2) Orodhesha gharama katika vikundi mbalimbali. Chakula, nyumba, gari, usafiri, na kadhalika.
(3) Tambua ni pesa ngapi ulizohifadhi utakazotumia kila mwezi kulipia matumizi ya kila kikundi kwenye orodha yako. Kwa ajili ya gharama za kila mwaka, “piga hesabu” ni pesa ngapi unazopaswa kuhifadhi kila mwezi.
(4) Andika jumla ya mapato yote ya kila mtu nyumbani. Ondoa malipo kama vile kodi. Linganisha na gharama.
(5) Tenga kiasi unachohitaji kila mwezi ili kulipia kila kikundi. Ikiwa unatumia pesa taslimu, njia rahisi ni kuwa na bahasha iliyo na alama ya kila kikundi. Kisha, tia pesa zinazohitajika ili kugharimia mahitaji hayo ndani ya kila bahasha.
Tahadhari: Ikiwa unatumia kadi ya mkopo, fanya hivyo kwa hekima! Bajeti za watu wengi zimevurugwa na tamaa ya ‘kununua sasa, kulipia baadaye.’
[Chati]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Mapato ya Mwezi
MSHAHARA WA MWEZI Sh.․․․․․ MAPATO MENGINE Sh.․․․․․
MSHAHARA WA WATU
WENGINE NYUMBANI Sh.․․․․․ JUMLA YA MAPATO HALISI
Sh.․․․․․
Gharama za Mwezi Pesa
Ulizopangia Ulizotumia
Sh.․․․․․ Kodi ya Nyumba Sh.․․․․․
Sh.․․․․․ Bima/Kodi Nyingine Sh.․․․․․
Sh.․․․․․ Gharama za Huduma Sh.․․․․․
Sh.․․․․․ Gharama za Gari Sh.․․․․․
Sh.․․․․․ Burudani/Usafiri Sh.․․․․․
Sh.․․․․․ Simu Sh.․․․․․
Sh.․․․․․ Chakula Sh.․․․․․
Sh.․․․․․ Gharama Nyingine Sh.․․․․․
JUMLA JUMLA
Sh.․․․․․ Sh.․․․․․
Linganisha na Matumizi
MAPATO YA MWEZI Sh.․․․․․
ONDOA− SALIO
MATUMIZI YA MWEZI Sh.․․․․․ Sh.․․․․․
-