Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Dhuluma Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2003 | Agosti 22
    • Ni nini maana ya kudhulumiwa? Mara nyingi dhuluma huhusisha matukio mengi madogo-madogo ambayo hufanywa kwa muda fulani bali si tukio moja au matukio machache tu. Dan Olweus, ambaye ni mtaalamu wa akili na mwanzilishi wa uchunguzi kuhusu dhuluma, anasema kwamba kwa kawaida dhuluma inahusisha kufanya ujeuri kimakusudi na kuwadhulumu watu wanyonge waziwazi.

      Huenda ufafanuzi wa neno dhuluma hauhusishi aina zote za dhuluma, lakini limefafanuliwa kuwa “kutaka kumuumiza mtu mwingine kimakusudi na kumfadhaisha.” Yule anayedhulumiwa hufadhaika anapotendewa vibaya au hata kwa sababu anaogopa yale atakayotendewa. Matendo hayo ni kama vile kumdhihaki, kumchambua kila wakati, kumtusi, kumsengenya, na kumshurutisha afanye mambo asiyoweza kufanya.—Ona sanduku kwenye ukurasa wa 4.

  • Dhuluma Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2003 | Agosti 22
    • [Sanduku katika ukurasa wa 4]

      Wadhalimu wa Aina Mbalimbali

      ◼ Wanaotumia Jeuri: Hawa ndio rahisi kutambua. Wanapokasirika wao humpiga mtu wanayemdhulumu, humsukuma, humpiga mateke, au kuharibu mali yake.

      ◼ Wanaotumia Matusi: Hawa hutumia maneno ili kuwaumiza au kuwaaibisha wengine kwa kuwabandika majina, kuwatukana, au kuwadhihaki tena na tena.

      ◼ Wanaoharibu Mahusiano: Hawa hueneza uvumi mbaya kuwahusu wengine. Wanawake wanaodhulumu wengine hupenda kutumia mbinu hii.

      ◼ Wanaolipiza Kisasi: Hawa ni watu ambao wamegeuka kuwa wadhalimu baada ya kudhulumiwa. Kudhulumiwa si udhuru wa kuwadhulumu wengine, bali kunatusaidia kuelewa kwa nini watu hao wamekuwa wadhalimu.

      [Hisani]

      Source: Take Action Against Bullying, by Gesele Lajoie, Alyson McLellan, and Cindi Seddon

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki