-
Kuhuburi na Kufundisha Ulimwenguni Pote2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Japani
Kwa sababu ya kuumwa na miguu, Hiroko mwenye umri wa miaka 78, hawezi kuhubiri kama zamani. Alisali ili apate mwongozo wa Mungu, na akapata kituo cha basi ambacho huwa na watu wengi ambapo anaweza kuketi kwa dakika 30. Yeye hutabasamu na kuwaonyesha watu urafiki. Kuna hospitali karibu, kwa hiyo akiwaona watu wamebeba dawa yeye huwauliza kuhusu afya yao. Ikiwa watu wanajaribu kusoma ratiba ya basi, yeye huwasaidia, na wale ambao hawafahamu eneo hilo, yeye huwaeleza sehemu zinazovutia. Yeye huwasikiliza wanapozungumza na kisha kuwapa magazeti. Yeye hukutana na baadhi ya watu hao kwa kawaida na hivyo anaweza kufanya ziara za kurudia.
-
-
Kuhuburi na Kufundisha Ulimwenguni Pote2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 53]
Hiroko akihubiri kwenye kituo cha basi
-