-
Je, Kweli Kuna Aina Yoyote ya Uhai Inayoweza Kuitwa Duni?Maswali Matano Muhimu Kuhusu Chanzo cha Uhai
-
-
Chembe hutumia muda mwingi kutengeneza protini. Inafanya hivyo jinsi gani? Kwanza, utaona chembe ikitengeneza kemikali za msingi 20 hivi zinazoitwa asidi-amino. Kemikali hizo za msingi hupelekwa hadi kwenye ribosomu (5), zinazoweza kulinganishwa na mashine zinazojiendesha zenyewe ambazo zinaunganisha asidi-amino katika utaratibu fulani ili kutengeneza protini hususa. Kama vile ambavyo huenda utendaji wote wa kiwanda ukaongozwa na programu ya kompyuta, utendaji mwingi wa chembe unaongozwa na “programu ya kompyuta” au molekuli ya DNA (6). Ribosomu hupokea kutoka kwa DNA nakala yenye maagizo kamili inayoiambia ni protini gani itakayotengeneza na jinsi ya kuitengeneza (7).
Kinachotokea protini inapotengenezwa ni chenye kustaajabisha! Kila moja hujikunja na kufanyiza umbo la kipekee lenye nyuso tatu (8). Umbo hilo ndilo linaloamua kazi hususa ambayo protini hiyo itafanya.b Wazia sehemu za injini zikiunganishwa pamoja. Kila sehemu inapaswa kutengenezwa kwa usahihi kabisa ili injini hiyo ifanye kazi. Vivyo hivyo, ikiwa protini haijatengenezwa kwa usahihi kamili na kukunjwa katika umbo hususa, haitaweza kufanya kazi yake vizuri na huenda hata ikaharibu chembe.
Protini inajuaje njia kutoka mahali ilipotengenezewa mpaka mahali inapohitajika? Kila protini inayotengenezwa na chembe inakuwa na “anwani” ili kuhakikisha kwamba protini hiyo itafika mahali inapohitajika. Ingawa maelfu ya protini hutengenezwa na kutumwa kila dakika, kila moja hufika mahali inapohitajika.
Kwa nini ukweli huu ni muhimu? Molekuli tata zilizo ndani ya vitu sahili vilivyo hai haziwezi kujizalisha. Zikiwa nje ya chembe, molekuli hizo hujigawanya. Zikiwa ndani ya chembe, haziwezi kujizalisha bila msaada wa molekuli nyingine tata. Kwa mfano, vimeng’enya vinahitajiwa ili kutengeneza molekuli ya pekee ya nishati inayoitwa adenosine triphosphate (ATP), hata hivyo, nishati kutoka kwa ATP inahitajika ili kutengeneza vimeng’enya. Vivyo hivyo, DNA (sehemu ya 3 inazungumzia molekuli hiyo) inahitajika ili kutengeneza vimeng’enya, hata hivyo, vimeng’enya vinahitajika ili kutengeneza DNA. Pia, protini nyingine zinaweza tu kutengenezwa na chembe, hata hivyo, chembe inafanyizwa kwa protini.c
-
-
Je, Kweli Kuna Aina Yoyote ya Uhai Inayoweza Kuitwa Duni?Maswali Matano Muhimu Kuhusu Chanzo cha Uhai
-
-
b Vimeng’enya ni kati ya protini zinazotengenezwa na chembe. Kila kimeng’enya hukunjwa kwa njia ya pekee ili kuharakisha utendaji hususa wa kemikali. Mamia ya vimeng’enya hushirikiana ili kudhibiti utendaji mbalimbali wa chembe.
c Baadhi ya chembe katika mwili wa mwanadamu zinafanyizwa na karibu molekuli 10,000,000,000 za protini11 ambazo ni mamia ya maelfu kadhaa ya aina tofauti-tofauti.12
-
-
Je, Kweli Kuna Aina Yoyote ya Uhai Inayoweza Kuitwa Duni?Maswali Matano Muhimu Kuhusu Chanzo cha Uhai
-
-
[Mchoro katika ukurasa wa 10, 11]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
“Kiwanda” cha Chembe
Jinsi Protini Zinavyotengenezwa
Kama kiwanda kinachojiendesha chenyewe, chembe imejaa mashini zinazokusanya na kusafirisha bidhaa tata
-