Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Chembe za Urithi, DNA, na Wewe
    Amkeni!—1999 | Septemba 8
    • Mwili wako umefanyizwa na sehemu hai ndogo-ndogo zinazoitwa chembe—zipatazo angalau trilioni 100, kulingana na kadirio moja. Katika kiini cha kila chembe, kuna maelfu ya chembe za urithi. Hizo ni sehemu mbalimbali za urithi zinazodhibiti chembe na kwa njia hiyo zinaamua baadhi ya tabia zako. Huenda chembe nyingi za urithi zikaamua aina ya damu yako; nyingine, umbile la nywele zako, rangi ya macho yako, na kadhalika. Kwa hiyo kila chembe hubeba maagizo katika chembe za urithi, maagizo yote yanayohitajiwa ili kujenga, kurekebisha, na kuelekeza utendaji wa mwili wako. (Ona mchoro, ukurasa wa 5.) Je, yote haya yaweza kuwa yalitukia kwa aksidenti?

  • Kuchunguza Chembe kwa Hadubini
    Amkeni!—1999 | Septemba 8
    • Hivyo wanasayansi wameona kwamba chembe ni tata ajabu. Katika kitabu chake The Fifth Miracle, mwanafizikia Paul Davies ataarifu hivi: “Kila chembe imejaa visehemu vidogo-vidogo ambavyo yaonekana viliundwa kwa kufuata kijitabu cha maagizo cha mhandisi. Kuna vibano, makasi, pampu, mota, nyenzo, vali, mifereji, minyororo, na hata magari mengi, vyote vikiwa vingi na vidogo sana. Bila shaka chembe si mfuko tu wa vitu. Sehemu mbalimbali huungana kufanyiza chembe moja inayotenda kazi kwa utaratibu, kama mashine iliyopangwa vyema kiwandani.”

  • Kuchunguza Chembe kwa Hadubini
    Amkeni!—1999 | Septemba 8
    • Uhai Ulianzia Wapi?

      Elimu ya urithi na biolojia ya molekuli imewakanganya wanasayansi kwa miongo mingi. Mwanafizikia Paul Davies anatilia shaka uwezekano wa kwamba Muumba ndiye aliyetokeza mambo haya yote. Ingawa hivyo, yeye akiri hivi: “Kila molekuli ina utendaji hususa na mahali pake hususa katika mpango wote hivi kwamba vitu vinavyofaa ndivyo vinavyofanyizwa. Kuna kusafiri kwingi kunakoendelea. Ni lazima molekuli zisafiri ndani ya chembe ili zikutane na nyingine mahali panapofaa na kwa wakati unaofaa ili ziweze kutekeleza kazi zake inavyofaa. Yote haya hutukia bila kuwapo kwa bwana-mkubwa anayeelekeza utendaji wa molekuli na kuzipeleka mahali panapofaa. Hakuna mwangalizi anayesimamia utendaji wao. Molekuli hufanya tu mambo ambayo molekuli zapaswa kufanya: kurukaruka bila utaratibu wowote, kugongana, kudundadunda, kukumbatiana. . . . Kwa njia fulani, na kwa pamoja, atomu hizi zisizokuwa na ufahamu huungana katika kucheza dansi ya uhai kwa utaratibu wa hali ya juu sana.”

      Wakiwa na sababu nzuri, watu wengi ambao wamechunguza utendaji ndani ya chembe wamekata kauli kwamba ni lazima kuwe na mtu mwenye akili aliyeumba chembe hii. Acheni tuone sababu.

  • Kuchunguza Chembe kwa Hadubini
    Amkeni!—1999 | Septemba 8
    • (Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

      Jinsi DNA Inavyojigawa

      Kwa kusudi la kuifanya ieleweke kwa urahisi, nyuzi za DNA zenye kujipinda zimenyooshwa

      1 Kabla chembe hazijajigawa ili kutokeza kizazi cha chembe kinachofuata, ni lazima zijigawe (zifanye nakala ya) DNA. Kwanza, protini husaidia kufumua sehemu za DNA yenye nyuzi mbili

      Protini

      2 Kisha, kwa kufuata sheria kali za muungano kwenye misingi, misingi iliyo huru (inayopatikana) katika chembe huungana pamoja na misingi inayolingana nayo kwenye nyuzi mbili za kwanza

      Misingi huru

      3 Hatimaye, nakala mbili za DNA hufanyizwa. Kwa hiyo, chembe inapojigawa, kila chembe mpya hupokea habari ileile ya DNA

      Protini

      Protini

      Sheria za muungano wa misingi ya DNA:

      Sikuzote A huungana na T

      A T Thymine

      T A Adenine

      Sikuzote C huungana na G

      C G Guanine

      G C Cytosine

      [Mchoro katika ukurasa wa 8, 9]

      (Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

      Jinsi Protini Zinavyofanyizwa

      Ili ieleweke kwa urahisi, tunatoa kielezi cha protini ambayo imefanyizwa kwa asidi-amino 10. Protini nyingi zina zaidi ya amino asidi 100

      1 Protini ya pekee hufunua sehemu ya nyuzi za DNA

      Protini

      2 Misingi huru ya RNA huungana na misingi iliyo wazi ya DNA kwenye uzi mmoja peke yake, na hilo hutokeza uzi wa RNA unaopeleka ujumbe

      Misingi huru ya RNA

      3 RNA yenye kupeleka ujumbe ambayo imetoka kufanyizwa huachana na DNA na kuelekea kwenye ribosomu

      4 RNA ya kuhamisha hubeba asidi-amino moja na kuipeleka kwenye ribosomu

      RNA inayohamisha

      Ribosomu

      5 Mnyororo wa asidi-amino huunganishwa pamoja wakati ribosomu inapopitia RNA inayopeleka ujumbe

      Asidi-amino

      6 Mnyororo wa protini unaofanyizwa huanza kujikunja katika umbo linalofaa ili kutekeleza kazi inavyofaa. Kisha mnyororo huo huachiliwa na ribosomu

      RNA ya kuhamisha ina sehemu mbili muhimu:

      Sehemu moja hutambua uzi wa RNA unaopeleka ujumbe

      Sehemu nyingine hubeba asidi-amino inayofaa

      RNA ya kuhamisha

      Misingi ya RNA hutumia U badala ya T, kwa hiyo U huungana na A

      A U Uracil

      U A Adenine

  • Uhai Ulianzaje?
    Amkeni!—1999 | Septemba 8
    • Uhai Ulianzaje?

      MOLEKULI ya DNA hutekeleza mambo ya kustaajabisha. DNA hutimiza mambo mawili yanayohitajiwa na chembe zako katika kufanyiza visehemu vya urithi. Kwanza, DNA hunakiliwa sawasawa ili habari iweze kupitishwa kutoka kwa chembe moja hadi nyingine. Pili, mfuatano wa DNA husaidia chembe kujua aina ya protini itakayofanyiza, na hivyo kuamua chembe hiyo itakuwa ya aina gani na kazi itakayofanya. Hata hivyo, DNA haitekelezi kazi hizi bila msaada. Protini nyingi za kipekee huhusika.

      DNA peke yake haiwezi kutokeza uhai. Ina maagizo yote yanayohitajiwa ili kufanyiza protini zote zinazohitajiwa na chembe hai, kutia ndani zile zinazonakili DNA kwa ajili ya kizazi kingine cha chembe na zile zinazosaidia DNA kufanyiza protini mpya. Ingawa hivyo, habari chungu nzima iliyohifadhiwa katika chembe za urithi za DNA ni bure pasipo RNA na protini za kipekee, zinazotia ndani ribosomu, zinazohitajiwa ili “kusoma” na kutumia habari hiyo.

      Wala protini peke yake haziwezi hutokeza uhai. Protini iliyo peke yake haiwezi kutokeza chembe ya urithi iliyo na maagizo ya kufanyiza protini za aina ileile.

      Kwa hiyo, kufumbua fumbo la uhai kumeonyesha nini? Elimu ya kisasa ya chembe za urithi na biolojia ya molekuli imetoa uthibitisho wa kutosha wa uhusiano ulio tata sana wenye kutegemeana kati ya DNA, RNA, na protini. Matokeo haya yanaonyesha kwamba uhai hutegemea kuwapo kwa elementi hizi zote kwa wakati mmoja. Hivyo, uhai haungeweza kamwe kutokea tu ghafula kwa nasibu.

      Maelezo pekee yanayopatana na akili ni kuwa Muumba mwenye akili sana aliweka maagizo katika DNA na wakati uleule akifanyiza protini zilizo kamili. Utendeano huo ulibuniwa kwa njia bora hivi kwamba mara tu baada ya kubuniwa, utendaji huu ungehakikisha kwamba protini zingeendelea kunakili DNA na kutokeza chembe zaidi za urithi, huku protini nyingine zikifasiri chembe hizi za urithi ili kufanyiza protini zaidi.

      Kwa wazi, utaratibu huu wa uhai wenye kustaajabisha ulianzishwa na Mbuni Mkuu, Yehova Mungu.

      Tumeumbwa kwa Njia ya Ajabu

      Ijapokuwa Biblia si kitabu cha kisayansi, inafunua mambo fulani kuhusu fungu la Muumba, aliyebuni maagizo ya uhai. Miaka elfu tatu hivi iliyopita, Mfalme Daudi wa Israeli, asiyejua lolote juu ya maendeleo ya kisasa katika utafiti wa urithi, alimwimbia hivi Muumba wake kwa lugha ya kishairi: “Ni wewe ndiwe uliyeumba mtima wangu, na kuniunganisha pamoja tumboni mwa mama yangu; ninakushukuru kwa sababu ya maajabu haya yote: kwa sababu ya umbo langu la ajabu, kwa sababu ya maajabu ya kazi zako. Unanijua kabisa, kwa kuwa uliona mifupa yangu ikiumbika nilipokuwa nikiumbwa kwa siri, nikishikanishwa pamoja ndani ya tumbo la uzazi.”—Zaburi 139:13-15, Jerusalem Bible.

      Hebu jiangalie sana katika kioo kwa muda tena. Angalia rangi ya macho yako, umbile la nywele zako, rangi ya uso wako, na umbo la ujumla la mwili wako. Fikiria jinsi mambo hayo yalivyorithiwa kutoka kwa vizazi vilivyopita na jinsi yanavyopitishwa kwa uzao wako. Sasa, fikiria Yule aliyepanga utaratibu huu wa kustaajabisha. Huenda ukasukumwa kurudia maneno yaliyoandikwa na mtume Yohana: “Wewe wastahili, Yehova, naam, Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu, kwa sababu uliumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako na vikaumbwa.”—Ufunuo 4:11.

      [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 10]

      Je, Ilitokana na Nasibu Tu?

      Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na wanasayansi wawili Waingereza unathibitisha kwamba msimbo wa urithi haukutokana na nasibu bila utaratibu maalum. “Uchunguzi wao umeonyesha kwamba [msimbo wa chembe za urithi] ni mojawapo ya misimbo bora kati ya mabilioni ya misimbo inayoweza kuwapo,” lasema gazeti New Scientist. Ni msimbo mmoja tu kati ya misimbo ya chembe za urithi takriban 1020 (1 ikifuatwa na sufuri 20) inayoweza kuwapo, uliochaguliwa mapema sana katika historia ya uhai. Mbona huu msimbo mahususi ukachaguliwa? Kwa sababu unapunguza kasoro zinazozuka wakati wa utengenezaji wa protini au kasoro zinazosababishwa na mabadiliko ya chembe za urithi. Yaani, msimbo huu hususa wa chembe za urithi unahakikisha kwamba sheria za urithi zinafuatwa kabisa. Ijapokuwa watu fulani hudai kwamba kuchaguliwa kwa msimbo huu kulitokana na “misongo yenye nguvu ya kuchagua,” watafiti hao wawili wamekata kauli kwamba “ni jambo lisilowezekana kabisa kwamba msimbo huu bora ulitokana na nasibu.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki