-
Kuzuia “Busu” la KifoAmkeni!—2000 | Septemba 8
-
-
Akukaribia usiku wa manane, ukiwa umelala fofofo. Hakuamshi. Wala huhisi chochote unapopewa “busu” lake lenye madhara.
MGENI huyu anayeingia usiku bila kukaribishwa ni mbawakavu aina ya barber ambaye husitawi Amerika Kusini—aitwaye pia mdudu abusuye. Mdudu huyo aweza kuendelea “kukubusu” kwa muda wa robo saa, huku akikunyonya damu polepole. “Busu” lenyewe halitakudhuru. Lakini kinyesi anachoacha ngozini mwako chaweza kuwa na kijiumbe kiitwacho Trypanosoma cruzi, au kwa ufupi T. cruzi. Kimelea hicho kikiingia mwilini mwako kupitia macho, mdomo, au kidonda, chaweza kusababisha maradhi ya American trypanosomiasis ambayo yajulikana kama maradhi ya Chagas.
-
-
Kuzuia “Busu” la KifoAmkeni!—2000 | Septemba 8
-
-
Imekadiriwa kwamba watu milioni 18 wameambukizwa maradhi ya Chagas, na watu 50,000 hufa kila mwaka kwa sababu ya maradhi hayo. Ugonjwa huo hauambukizwi kwa kuumwa tu na mdudu huyo. Kwa mfano, baadhi ya walioambukizwa ni watoto walionyonyeshwa, ambao waliambukizwa na mama zao wenye ugonjwa huo. Mwanamke mjamzito hata aweza kumwambukiza mtoto wake tumboni, au kumwambukiza anapojifungua. Njia nyingine za kuambukizwa ni kupitia kutiwa damu mishipani au kula chakula kisichopikwa ambacho kimechafuliwa kwa kijiumbe cha T. cruzi.b
-