-
Kutafuna Chingamu Ni Zoea la Kisasa na la KaleAmkeni!—2002 | Februari 22
-
-
Kwa nini chingamu hupendwa sana? Wengi hutafuna chingamu ili kusafisha pumzi na kusafisha meno baada ya kula, wakiwa mahali ambapo hawawezi kutumia mswaki.a Wengine hutafuna chingamu ili kutulia au kukaza fikira kwenye jambo fulani. Kwa kuwa kutafuna chingamu humtuliza mtu na kumsaidia kukaa chonjo, wanajeshi wa Marekani walipewa chingamu wakati wa vita ya kwanza na ya pili ya ulimwengu, na bado ni sehemu ya posho ambayo wanajeshi walio vitani hupewa. Baadhi ya madereva huona kwamba kutafuna chingamu huwasaidia sana kukaa macho kuliko kunywa kahawa. Kutafuna chingamu huwasaidia watu wanaojaribu kuacha kuvuta sigara. Pia inapendwa kama kibadala cha vitafunio, kwa kuwa kipande kimoja cha chingamu kina kalori kumi hivi.
-
-
Kutafuna Chingamu Ni Zoea la Kisasa na la KaleAmkeni!—2002 | Februari 22
-
-
Kutafuna chingamu huongeza mate, nayo huondoa asidi kwenye meno, na hivyo kudumisha afya bora mdomoni na kuzuia meno yasioze. Madaktari wa meno wanapendekeza kwamba chingamu isiyo na sukari itumiwe kwa kusudi hilo.
-