-
‘Weka Moyoni Mwako’ Hekalu la Mungu!Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
8. (a) Ni nani waliokuwa wakuu wa Israeli la kale? (b) Mkuu aliye katika ono la Ezekieli alikuwa mtendaji katika ibada safi kwa njia zipi?
8 Ono hilo pia humrejezea mmoja aitwaye mkuu. Tangu siku za Musa, taifa hilo lilikuwa na wakuu. Neno la Kiebrania linalotafsiriwa mkuu, yaani na·siʼʹ, lingeweza kurejezea kichwa cha jamaa ya upande wa baba, cha kabila, au hata cha taifa. Katika ono la Ezekieli, watawala wa Israeli wakiwa jamii wanakemewa kwa kuwaonea watu na wanahimizwa sana wasipendelee na wawe wenye haki. Ijapokuwa yeye si wa jamii ya kikuhani, mkuu huyo ni mtendaji kwa njia yenye kutokeza katika ibada safi. Yeye aingia na kutokea ua wa nje akiwa pamoja na yale makabila yasiyo ya kikuhani, aketi kwenye ukumbi wa Lango la Mashariki, na kuandaa baadhi ya dhabihu ili watu wazitoe. (Ezekieli 44:2, 3; 45:8-12, 17) Hivyo, ono hilo liliwahakikishia watu wa Ezekieli kwamba taifa lililorudishwa lingebarikiwa kwa kupewa viongozi wenye kielelezo kizuri, wanaume ambao wangetegemeza ukuhani katika kusimamia watu wa Mungu na kuwa vielelezo bora katika mambo ya kiroho.
-
-
‘Weka Moyoni Mwako’ Hekalu la Mungu!Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
Yule mkuu vilevile angepata urithi. Lakini makuhani hawangepata urithi, kwa kuwa Yehova alisema, “Mimi ni urithi wao.” (Ezekieli 44:10, 28; Hesabu 18:20) Ono hilo lilionyesha kwamba sehemu ya nchi iliyogawiwa yule mkuu ingekuwa kila upande wa eneo la pekee liitwalo toleo takatifu.
-
-
‘Weka Moyoni Mwako’ Hekalu la Mungu!Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
Na ona kwamba katika ono la Ezekieli mkuu huyo, sawa na makuhani, angeishi katika sehemu ya nchi iliyotolewa na watu. (Ezekieli 45:16) Kwa hiyo, katika nchi iliyorudishwa, watu walipaswa kuchangia kazi ya wale ambao Yehova alichagua waongoze, wakiwaunga mkono kwa kukubali mwelekezo wao. Kwa ujumla, nchi hiyo ilikuwa mfano mzuri wa utaratibu, ushirikiano, na usalama.
-
-
‘Weka Moyoni Mwako’ Hekalu la Mungu!Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
Wakuu, kama vile Nehemia na Zerubabeli, walitawala nchi hiyo bila upendeleo na kwa haki.
-