Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Unaweza Kufanikiwa Licha ya Malezi Yako
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 15
    • Malinda, aliyetajwa mapema, alikuwa na jirani mzee mwenye fadhili aliyeleta magazeti ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni kwa ukawaida nyumbani kwao! Anapomfikiria jirani huyo kwa upendo, anasema hivi: “Jambo ambalo lilinivutia sana kuhusu jirani yangu lilikuwa kwamba hakusherehekea sikukuu. Jambo hilo lilikuwa muhimu kwangu kwa kuwa sikukuu ya Halloween (sherehe ya usiku wa tarehe 30 ya Oktoba) na baadhi ya sikukuu nyingine zilikuwa vipindi vya kufuatia desturi za madhehebu ya wazazi wangu.” Miaka kumi baadaye, rafiki ya Malinda alipomwalika kuhudhuria mkutano wa Kikristo kwenye Jumba la Ufalme la Mashahidi wa Yehova, alimkumbuka jirani huyo, naye akakubali mwaliko huo bila kusita. Jambo hilo lilimsaidia kupata ukweli.

  • Unaweza Kufanikiwa Licha ya Malezi Yako
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 15
    • Malinda pia huwaendea wazee anapohitaji kufanya maamuzi muhimu maishani. Anapokabiliana na hisia ya kukata tamaa na kujihisi kuwa duni, hisia ambazo zilianza utotoni, kile ambacho humsaidia hasa ni makala mbalimbali za magazeti ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Anasema hivi: “Nyakati nyingine katika makala kuna fungu moja tu au sentensi—sehemu ndogo sana—ambayo hunisaidia. Yapata miaka tisa iliyopita nilianza kuweka makala hizo katika jalada, ili niweze kuzirejea kwa urahisi.” Kwa sasa, ana vitabu vitatu vyenye makala 400 hivi!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki