-
Linda Dhidi ya Kutopenda KusomaAmkeni!—1996 | Januari 22
-
-
Vyema hata zaidi, wazazi fulani husomea watoto wao vitabu kwa sauti kubwa. Kwa kufanya hilo, wao hukuza kifungo kichangamfu—kitu ambacho, kwa kuhuzunisha kinakosekana katika familia nyingi leo.
-
-
Linda Dhidi ya Kutopenda KusomaAmkeni!—1996 | Januari 22
-
-
Wazazi fulani huanza kuwasomea watoto wao vitabu katika umri mchanga. Hili laweza kuwa na manufaa. Wataalamu fulani husema kwamba kufikia umri wa miaka mitatu, mtoto hufahamu sehemu kubwa ya lugha atakayotumia katika mazungumzo ya kawaida ya watu wazima—hata ingawa hawezi bado kueleza maneno haya kwa ufasaha. “Watoto huanza kujifunza kufahamu lugha mapema zaidi na kwa kiwango cha haraka zaidi kuliko wajifunzavyo kuitumia kwa usemi,” chasema kitabu The First Three Years of Life. Biblia husema hivi kumhusu Timotheo: “Tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu.” (2 Timotheo 3:15) Neno kitoto hurudi nyuma hadi kwenye neno la Kilatini infans, ambalo kihalisi humaanisha “asiyeongea.” Ndiyo, Timotheo alisikiliza maneno ya kimaandiko muda mrefu kabla ya kuweza kuyaongea.
-