Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wahama-Hamaji wa Asia Waliofanyiza Milki
    Amkeni!—2008 | Mei
    • Ng’ambo ya Mongolia

      Eneo la kaskazini mwa China lilikaliwa na Manchu, ambao waliita milki yao Jin, au “Ya Kidhahabu.” Ili kufika katika maeneo ya Manchu, Wamongol walivuka Jangwa la Gobi linalotisha, lakini hilo halikuwa tatizo kubwa kwa wahama-hamaji ambao, ikiwa lazima, wangeweza kuishi kwa kunywa tu maziwa na damu ya farasi. Ijapokuwa Genghis Khan alipanua utawala wake utie ndani China na Manchuria, vita viliendelea kwa miaka 20 hivi. Alichagua baadhi ya Wachina waliokuwa wasomi, wasanii, wafanyabiashara, na pia wahandisi ambao wangeweza kujenga kuta za mazingiwa, manati, na mabomu ya unga wa risasi.

  • Wahama-Hamaji wa Asia Waliofanyiza Milki
    Amkeni!—2008 | Mei
    • Ögödei alidhibiti tena maeneo yaliyokuwa yametiishwa, akapokea ushuru kutoka kwa vibaraka, na kumaliza milki ya Jin huko kaskazini mwa China.

      Ili kuendeleza milki na mtindo wa starehe wa maisha ambao Wamongol walikuwa wamezoea, hatimaye Ögödei kwenda vitani tena—lakini wakati huu alitaka kupigana na nchi ambazo hawakuwa wamezitiisha. Alishambulia maeneo mawili tofauti—nchi za Ulaya upande wa magharibi na milki ya Sung kusini mwa China. Kampeni ya Ulaya ilifanikiwa, lakini ya China haikufanikiwa. Ijapokuwa walipata mafanikio fulani, Wamongol hawakufaulu kutiisha eneo kuu la Sung.

  • Wahama-Hamaji wa Asia Waliofanyiza Milki
    Amkeni!—2008 | Mei
    • Mashambulio Mengine Katika Maeneo Mawili

      Khan Mkuu aliyefuata alikuwa Mongke, ambaye alitawazwa mnamo 1251. Yeye na nduguye Kublai walishambulia milki ya Sung kusini mwa China, huku jeshi lingine likishambulia maeneo ya magharibi.

  • Wahama-Hamaji wa Asia Waliofanyiza Milki
    Amkeni!—2008 | Mei
    • Mashambulizi yaliyofanywa kusini mwa China dhidi ya milki tajiri ya Sung yalifanikiwa. Kublai Khan alijitangaza kuwa mwanzilishi wa milki mpya ya China, na kuiita Yuan. Jiji kuu la milki hiyo leo linaitwa Beijing. Baada ya kuwashinda wale ambao bado walikuwa wakiunga mkono milki ya Sung mwishoni mwa miaka ya 1270, Kublai alitawala China iliyounganishwa kwa mara ya kwanza tangu kuanguka kwa milki ya Tang mnamo 907.

  • Wahama-Hamaji wa Asia Waliofanyiza Milki
    Amkeni!—2008 | Mei
    • Huko China, mapambano ya kushindania utawala yalipunguza mamlaka ya wazao wa Kublai. Katika 1368 Wachina, waliochoshwa na utawala mbaya, ufisadi, na kodi kubwa, waliwapindua mabwana wao wa milki ya Yuan, na kuwafurusha warudi Mongolia.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki