-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
8, 9. (a) Vatikani na pia Kanisa Katoliki na viongozi wa kidini wayo walitendaje katika kuitikia ukatili wa Nazi? (b) Ni taarifa gani ambayo Maaskofu Wakatoliki wa Ujeremani walitoa mwanzoni mwa Vita ya Ulimwengu 2? (c) Mahusiano ya dini-siasa yamekuwa na matokeo gani?
8 Ingawa mapadri na watawa wa kike wachache waliteta dhidi ya matendo ya ubahaimu ya Hitla—na wakapata mateso kwa kufanya hivyo—Vatikani pamoja na Kanisa Katoliki na jeshi layo la viongozi wa kidini waliunga mkono ukatili wa Nazi ama kwa vitendo au kwa kutoteta, waliuona kuwa kinga dhidi ya kusonga mbele kwa Ukomunisti wa ulimwengu. Akijikalia kitako katika Vatikani, Papa Pius 12 aliachilia Uharibifu Mkubwa wa Wayahudi na unyanyaso wa ukatili juu ya Mashahidi wa Yehova na wengine uendelee bila kuchambuliwa. Ni kinyume kwamba Papa John Paul 2, alipozuru Ujeremani katika Mei 1987, alipaswa kutukuza msimamo wa padri mmoja mwenye moyo mweupe wa kupinga Unazi. Yale maelfu mengine ya viongozi wa kidini wa Ujeremani walikuwa wakifanya nini wakati wa utawala wa kuogofya wa Hitla? Barua moja ya uchungaji iliyotolewa na maaskofu wa Ukatoliki wa Ujeremani katika Septemba 1939 ilipotokea Vita ya Ulimwengu 2, inatoa nuru juu ya jambo hili. Kwa sehemu inasomwa hivi: “Katika saa hii ya kukata maneno sisi twashauri askari-jeshi Wakatoliki kufanya wajibu wao katika utii kwa Fuehrer na kuwa tayari kudhabihu nafsi nzima yao. Sisi tunasihi Waaminifu wajiunge katika sala zenye idili kwamba huu Mwongozo wa Kimungu uweze kupeleka vita hii kwenye ufanisi wenye baraka.”
-
-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 238]
Chini ya kichwa hiki, makala inayofuata ilitokea katika chapa ya kwanza ya The New York Times ya Desemba 7, 1941:
‘SALA YA VITA’ KWA AJILI YA REICH
Maaskofu wa Kikatoliki katika Fulda Waomba Baraka na Ushindi
Kongamano la Maaskofu wa Kikatoliki wa Ujeremani lililokusanyika katika Fulda limependekeza ianzishwe ‘sala ya vita’ maalumu ambayo itasomwa mwanzoni na mwishoni mwa ibada zote za kimungu. Sala hiyo husihi Mungu abariki silaha za Ujeremani kwa ushindi na kutoa himaya kwa maisha na afya ya askari-jeshi wote. Maaskofu hao waliwaagiza zaidi makasisi wa Kikatoliki waweke na kukumbuka katika mahubiri maalumu ya Jumapili angalau mara moja kwa mwezi askari-jeshi Wajeremani ‘barani, baharini na hewani.’”
Makala hii iliondolewa kwenye chapa za baadaye za nyusipepa hiyo. Desemba 7, 1941, ndiyo siku Japani, nchi fungamani na Ujeremani, iliposhambulia meli za U.S. kwenye Pearl Harbor.
[Picha katika ukurasa wa 244]
“Majina ya Kufuru”
Hayawani-mwitu mwenye pembe mbili alipoendeleza Ushirika wa Mataifa baada ya Vita ya Ulimwengu 1, hawara zake wa kidini walitafuta mara hiyo kulipa tendo hilo idhini ya kidini. Kama tokeo, tengenezo jipya la amani ‘likajawa na majina ya kufuru.’
-