-
Makanisa Yanaelekea Wapi?Amkeni!—2007 | Februari
-
-
Makanisa Yanaelekea Wapi?
MAKANISA yanayodai kuwa ya Kikristo yanapatwa na nini? Mahali unapoishi, je, idadi ya watu wanaoenda kanisani inapungua au inaongezeka? Mara kwa mara utasikia madai ya kwamba watu wameanza tena kupendezwa na dini, na ripoti za makanisa kufurika watu huko Afrika, Ulaya Mashariki na Marekani. Hata hivyo, ripoti kutoka sehemu nyingine za ulimwengu, hasa Ulaya Magharibi, zinaonyesha kwamba makanisa yanafungwa, idadi ya watu wanaoenda kanisani inapungua, na watu wengi hawapendezwi na dini.
Kwa sababu ya kupungua kwa wahudhuriaji, makanisa mengi yamebadilisha mitindo yao. Mengine yanadai “hayamhukumu” mtu yeyote na hivyo kuonyesha kwamba Mungu hukubali mwenendo wowote. Isitoshe, badala ya kufundisha Neno la Mungu, makanisa mengi yanaandaa burudani na vivutio vingine visivyohusiana na dini. Ingawa waumini fulani wanaona mabadiliko hayo kuwa yanafaa katika ulimwengu huu wa kisasa, watu wengi wanyofu wanajiuliza ikiwa makanisa yanakengeuka kutoka kwenye utume ambao Yesu aliyapa. Acheni tuchunguze mwelekeo ambao makanisa yamechukua katika miaka ya karibuni.
-
-
Makanisa Yanapatwa na Nini?Amkeni!—2007 | Februari
-
-
Makanisa Yanapatwa na Nini?
WATU wanaoishi Brazili na katika nchi za Amerika zinazozungumza Kihispania, kutoka Mexico upande wa kaskazini hadi Chile upande wa kusini, wana utamaduni unaofanana. Wazee wanaoishi katika maeneo hayo hukumbuka wakati ambapo kulikuwa na dini moja tu, dini ya Katoliki. Katika karne ya 16, wakoloni wa Hispania walitumia silaha kuwalazimisha watu kuwa Wakatoliki. Brazili ilikuwa koloni ya Ureno iliyofuata Ukatoliki. Kwa miaka 400, Kanisa Katoliki liliunga mkono serikali iliyokuwa inatawala ili ipate msaada wa kifedha na kutambuliwa kuwa dini rasmi.
Lakini katika miaka ya 1960, baadhi ya makasisi Wakatoliki waligundua kwamba kuunga mkono wanaotawala kunawafanya wasipendwe na watu wengi. Hivyo, wakaanza kampeni ya kuwaunga mkono watu maskini, kwa kuanzisha kile kilichoitwa harakati ya Kanisa Katoliki ya kuleta mabadiliko ya kijamii na kutetea haki za kibinadamu. Harakati hiyo ilianzia Brazili na katika nchi za Amerika zinazozungumza Kihispania ili kulalamika kuhusu hali ya umaskini ya Wakatoliki wengi.
Licha ya jitihada za makasisi za kujiingiza katika harakati za siasa zinazopendwa, bado mamilioni ya watu wameacha Ukatoliki na kujiunga na makanisa mengine. Dini ambazo ibada yao inatia ndani kupiga makofi na kuimba nyimbo za dini kwa hisia au zilizo na makelele kama maonyesho ya muziki wa roki zimeongezeka sana. Duncan Green, anasema hivi katika kitabu chake Faces of Latin America: “Harakati ya Kievanjeli huko Brazili na katika nchi za Amerika zinazozungumza Kihispania imegawanyika na kuwa makanisa mengi mbalimbali. Makanisa mengi kati ya hayo huanzishwa na mchungaji mmoja ambaye ndiye huongoza mambo yote. Mara nyingi, waumini wanapoongezeka, kanisa hugawanyika na kuwa Makanisa mengi mapya.”
Ulaya Yapuuza Makanisa
Kwa zaidi ya miaka 1,600, nchi nyingi za Ulaya zimetawaliwa na serikali zilizodai kuwa za Kikristo. Je, dini huko Ulaya zinazidi kusitawi katika karne hii ya 21? Katika mwaka wa 2002, mwanasosholojia Steve Bruce, alisema hivi kuhusu Uingereza katika kitabu chake God is Dead—Secularization in the West: “Katika karne ya 19 karibu ndoa zote zilifungiwa kanisani.” Lakini kufikia mwaka wa 1971, ni asilimia 60 za ndoa zilizofungiwa kanisani na kufikia mwaka wa 2000, zilikuwa asilimia 31 tu.
Akizungumzia mwelekeo huo, mwandishi mmoja wa mambo ya kidini wa gazeti la London la Daily Telegraph aliandika hivi: “Makanisa yote makubwa kuanzia Kanisa la Anglikana, Katoliki, Methodisti, na makanisa ya United Reformed, yamekuwa na upungufu mkubwa sana wa waumini kwa muda mrefu.” Aliendelea kusema hivi: “Makanisa ya Uingereza yatakuwa yakikaribia kutoweka kufikia mwaka wa 2040 na asilimia mbili tu ya watu ndio watakaokuwa wakihudhuria ibada ya Jumapili.” Kumekuwa na ripoti kama hizo pia kuhusu dini huko Uholanzi.
“Katika miaka ya hivi karibuni, inaonekana kwamba nchi yetu imeaanza kufuatia sana mambo ya kimwili,” ikasema ripoti moja ya Ofisi ya Uholanzi ya Kupanga Masuala ya Kijamii na Kitamaduni. “Inatazamiwa kwamba kufikia mwaka wa 2020, asilimia 72 ya watu nchini humu hawatakuwa wakijihusisha kwa njia yoyote na mambo ya kidini.” Gazeti moja la Ujerumani linasema hivi: “Wajerumani wengi wanageukia uchawi na mizungu ili kupata kitulizo walichokuwa wakipata makanisani, kazini, na katika familia. . . . Makanisa mengi nchini Ujerumani yanalazimika kufungwa kwa kukosa waumini.”
Wale wanaoenda kanisani huko Ulaya hawaendi huko ili kujua yale ambayo Mungu anataka wafanye. Ripoti moja kutoka Italia ilisema: “Waitaliano huchagua dini ambayo inapatana na mapendezi yao.” Mwanasosholojia mmoja huko alisema hivi: “Tunakubali kutoka kwa papa yale ambayo yanatupendeza.” Mambo kama hayo yanaweza kusemwa kuhusu Wakatoliki huko Hispania, ambako watu wameacha kuwa na bidii ya mambo ya dini na badala yake wanafuatilia vitu vya kimwili ambavyo mtu anaweza kuvipata sasa.
Mielekeo hiyo inatofautiana sana na Ukristo ambao Kristo na wafuasi wake walifundisha na kufuata. Yesu hakufundisha kwamba dini ni kama meza yenye vyakula mbalimbali ambapo mtu anaweza kuchagua kile anachopenda na kuacha kile ambacho hapendi. Alisema hivi: “Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe na kuuchukua mti wake wa mateso siku baada ya siku na kunifuata sikuzote.” Yesu alifundisha kwamba maisha ya Kikristo yanahusisha kujidhabihu na kujitahidi.—Luka 9:23.
Mbinu za Kuvuta Watu Kwenye Dini Huko Amerika Kaskazini
Tofauti na hali ilivyo huko Kanada ambako wachunguzi wanasema kuwa watu wana mwelekeo wa kushuku dini, watu huko Marekani wana mwelekeo wa kuchukua mambo ya kidini kwa uzito. Kulingana na uchunguzi uliofanywa na baadhi ya mashirika makubwa ya kutafuta maoni, asilimia 40 hivi ya watu hudai kwamba wao huenda kanisani kila juma, ingawa idadi ya waliohesabiwa ilionyesha kwamba watu karibu asilimia 20 tu ndio hufanya hivyo. Zaidi ya asilimia 60 husema wanaamini kwamba Biblia ni Neno la Mungu. Hata hivyo, shauku yao kuelekea dini fulani huwa ya muda tu. Waumini wengi huko Marekani hubadili dini yao haraka. Mhubiri akipoteza umaarufu au uvutano wake, anaweza kupoteza waumini na pia mapato yake!
Makasisi fulani wanajifunza njia za kibiashara ili waone jinsi ya kuboresha mbinu za kuwavuta watu kwenye ibada zao. Makanisa hulipa mashirika yenye kutoa ushauri maelfu ya dola ili kupata ushauri. Kulingana na ripoti moja kuhusu mashirika hayo, mchungaji mmoja aliyeridhika na mpango huo alisema hivi: “Mpango huo ulileta faida kubwa.” Makanisa makubwa sana yenye maelfu ya waumini, yanapata faida nyingi hivi kwamba yanavuta uangalifu wa majarida ya mambo ya biashara kama vile The Wall Street Journal na The Economist. Majarida hayo yanasema kwamba makanisa makubwa sana huwa “mahali ambapo watu wanaweza kutosheleza mahitaji yao ya kimwili na ya kiroho.” Ndani ya majengo hayo kunakuwa na mikahawa, saluni, sauna, na mahali pa michezo. Vivutio vinatia ndani michezo ya kuigiza, maonyesho ya watu mashuhuri, na muziki wa kisasa. Lakini, makasisi wake wanafundisha nini?
Haishangazi kwamba wao hupenda kuhubiri ‘injili ya ufanisi.’ Waumini huambiwa kwamba watatajirika na kupata afya nzuri wakitoa sadaka nyingi. Kuhusiana na maadili, wanadai kwamba Mungu hukubali mwenendo wowote. Mwanasosholojia mmoja anasema hivi: “Makanisa ya Marekani hayahukumu mwenendo wa mtu bali hutoa kitulizo.” Mara nyingi dini zinazopendwa sana hukazia jinsi mtu anavyoweza kujisaidia mwenyewe na kufanikiwa maishani. Idadi inayozidi kuongezeka ya watu wanapendelea kuwa wafuasi wa makanisa ambayo hayashirikiani na dini fulani hususa, na ambayo hayazungumzii mafundisho yanayoonwa kuwa yenye kugawanya. Hata hivyo, mambo hususa ya kisiasa huzungumziwa waziwazi. Visa vya hivi karibuni vya makanisa hayo kujiingiza katika siasa vimewaaibisha makasisi fulani.
Je, watu huko Amerika ya Kaskazini wameanza kupendezwa tena na dini? Mnamo 2005, gazeti Newsweek liliripoti kuhusu umaarufu wa desturi za kidini zilizotia ndani “kupiga kelele, kuzirai, kukanyaga-kanyaga miguu chini kwa kishindo,” lakini gazeti hilo linaendelea kusema: “Chochote kinachoendelea hapa si ongezeko kubwa la watu wanaoenda kanisani.” Kulingana na uchunguzi uliofanywa, idadi ya watu wanaosema hawashirikiani na dini fulani hususa imeongezeka sana. Idadi ya waumini katika makanisa fulani inaongezeka kwa sababu idadi ya waumini katika makanisa mengine inapungua. Inadaiwa kwamba halaiki ya watu wanaacha dini za zamani zilizokuwa na muziki wa kinanda, makasisi wenye majoho rasmi, na sherehe fulani.
Kwa ufupi tumezungumzia jinsi makanisa yanavyogawanyika huko Brazili na katika nchi za Amerika zinazozungumza Kihispania, jinsi yanavyopoteza waumini huko Ulaya, na jitihada zake za kuwavutia waumini kwa kuandaa burudani na vivutio huko Marekani. Bila shaka, si kila mahali hali iko hivyo, lakini makanisa kwa ujumla yanajaribu kudumisha uvutano wake. Je, hilo linamaanisha kwamba Ukristo unaporomoka?
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 6]
“WATU WANACHAGUA-CHAGUA DINI KAMA BIDHAA”
Mkurugenzi wa Kituo cha Ufundi cha Kitaifa cha Kanisa Katoliki huko Ufaransa, alinukuliwa akisema hivi: “Tunaona watu wakichagua-chagua dini kama bidhaa kwenye maduka makubwa. Watu wanakuwa waumini wa kanisa fulani kwa muda, kisha wakiona haliwafai wanahamia lingine.” Profesa Grace Davie wa Chuo Kikuu cha Exeter huko Uingereza alisema hivi katika uchunguzi aliofanya kuhusu dini huko Ulaya: “Watu wanachagua na kuchanganya mafundisho kutoka dini mbalimbali. Dini imekuwa kama bidhaa nyingine ambazo watu huchagua wanachotaka kwa kutegemea mtindo wao wa maisha na mapendezi.”
[Picha katika ukurasa wa 4, 5]
Ukuta uliochorwa-chorwa katika mlango wa kanisa, Naples, Italia
[Hisani]
©Doug Scott/age fotostock
[Picha katika ukurasa wa 4, 5]
Watu wengi wameacha Ukatoliki
-
-
Kuna Tumaini Gani kwa Ukristo?Amkeni!—2007 | Februari
-
-
Kuna Tumaini Gani kwa Ukristo?
JE, WATU wote duniani watageuzwa kuwa Wakristo, au Ukristo utatokomea? Je, Ukristo ulibaki ukiwa nuru nyangavu katika ulimwengu wenye giza, au ulipotoshwa? Hayo ni maswali yanayotusumbua hadi leo.
Akitumia mfano unaoeleweka kwa urahisi, Yesu alionyesha kwamba mara tu baada ya yeye kupanda mbegu za Ukristo, adui, Shetani angeharibu mambo. (Mathayo 13:24, 25) Hivyo si mwelekeo wa kijamii uliofanya Ukristo ubadilike katika karne za mapema baada ya huduma ya Yesu, bali ni kitendo kiovu cha adui Shetani. Leo makanisa ya Jumuiya ya Wakristo yanaendeleza makosa yaliyofanywa zamani na yanavuna matokeo yake.—2 Wakorintho 11:14, 15; Yakobo 4:4.
Ukristo Washambuliwa kwa Hila
Yesu alitabiri kwamba mafundisho yake yangepotoshwa. Alisema: “Ufalme wa mbinguni umekuwa kama mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. Watu wakiwa wamelala usingizi, adui yake alikuja na kupanda magugu katikati ya ngano, naye akaondoka.” Kwa kushangaza watumishi walipomweleza kuhusu tendo hilo ovu na kuomba ruhusa wakusanye magugu, mtu huyo aliwaambia hivi: “Hapana; ili, mnapoyakusanya magugu, msije mkang’oa ngano pamoja nayo. Acheni zikue pamoja mpaka wakati wa mavuno; na katika majira ya mavuno nitawaambia wavunaji, Kwanza kusanyeni magugu na kuyafunga matita-matita ili kuyateketeza motoni, ndipo nendeni mkusanye ngano ghalani mwangu.”—Mathayo 13:24-30.
Kama Yesu mwenyewe alivyofafanua kwenye mfano wake, mtu aliyepanda ngano katika shamba anawakilisha Yesu, na mbegu alizopanda zinawakilisha Wakristo wa kweli. Adui aliyepanda magugu miongoni mwa ngano anawakilisha “Ibilisi.” Magugu yanawakilisha waasi-sheria na waasi-imani ambao walidai kuwa watumishi wa Mungu. (Mathayo 13:36-42) Mtume Paulo aliendelea kueleza kile ambacho kingetokea. Alisema hivi: “Ninajua kwamba baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wenye kukandamiza wataingia katikati yenu nao hawatalitendea kundi kwa wororo, na kutoka katikati yenu ninyi wenyewe watu watasimama na kusema mambo yaliyopotoka ili kuwavuta wanafunzi wawafuate wao wenyewe.”—Matendo 20:29, 30.
Ukristo Wapotoshwa
Je, mfano ambao Yesu alitoa na yale ambayo Paulo alitabiri yalitimia? Ndiyo yalitimia. Wanaume wenye kujitakia makuu walilitumia kutaniko ambalo Yesu alianzisha kwa faida yao wenyewe. Yesu alikuwa amewaambia wafuasi wake hivi: “Ninyi si sehemu ya ulimwengu.” (Yohana 15:19) Hata hivyo, watu wenye pupa ya mamlaka walifanya mapatano na viongozi wa serikali na makanisa yao yaliyoungwa mkono na Serikali yakajikusanyia mamlaka makubwa na utajiri mwingi. Makanisa hayo yalifundisha “mambo yaliyopotoka.” Kwa mfano, yalifundisha watu kuabudu Serikali na kudhabihu maisha yao vitani. Wale waliojiita Wakristo walijihusisha katika Vita Vitakatifu na kuwaua watu waliowaona kuwa si waamini. Pia walipigana vitani na kuwaua “ndugu” zao, yaani, waumini wenzao. Kwa kweli, hawakuwapenda jirani zao wala kudumisha msimamo wa kutounga mkono siasa.—Mathayo 22:37-39; Yohana 15:19; 2 Wakorintho 10:3-5; 1 Yohana 4:8, 11.
Kwa wazi, makanisa ambayo kwa karne nyingi yamejiita ya Kikristo yanawakilisha Ukristo bandia. Kama tulivyoona katika makala zilizotangulia, hiyo ndiyo sababu kumekuwa na mwelekeo wa makanisa kugawanyika na kuwa madhehebu, kujihusisha katika siasa, na kupuuza sheria za Mungu. Matunda hayo mabaya hayakutokezwa na Ukristo wa kweli bali ni matokeo ya Ukristo bandia ambao Ibilisi alipanda. Dini hiyo ya uwongo inaelekea wapi? Kama Yesu alivyoonyesha katika mfano wake, dini hiyo haitatokomea tu kwa kukosa waumini. Itahukumiwa na kuharibiwa.
-