-
Kuchunguza Rangi na Vitambaa Nyakati za BibliaMnara wa Mlinzi—2012 | Machi 1
-
-
Mara ya kwanza Biblia inapotaja kitani ni wakati inaporejelea mavazi ambayo Farao alimvisha Yosefu katika karne ya 18 K.W.K. (Mwanzo 41:42)
-
-
Kuchunguza Rangi na Vitambaa Nyakati za BibliaMnara wa Mlinzi—2012 | Machi 1
-
-
Kitani ni aina ya kitambaa kilichopendwa sana ambacho kilitengenezwa kwa nyuzi za mmea wa kitani. (Kutoka 9:31) Mmea huo ulivunwa wakati ulipokuwa karibu kukomaa kabisa. Shina la mmea huo lilikaushwa kwa jua kisha likaloweshwa ndani ya maji ili kulainisha sehemu zake ngumu. Baada ya kukaushwa, shina hilo lingepigwa-pigwa na nyuzi zake kutenganishwa, kisha kusokotwa ili kutokeza nyuzi zilizotumiwa kufuma. Watu wa familia ya kifalme na maafisa wa ngazi za juu walipendelea mavazi yaliyotengenezwa kwa kitani.
[Picha]
Mmea wa kitani uliokaushwa kabla ya kuloweshwa
-