-
Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye TamatiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Tazama! Mimi ninakuja kama mwivi. Mwenye furaha ni mmoja ambaye hukaa ameamka na kutunza mavazi yake ya nje, ili asipate kutembea uchi na watu watazame aibu yake.” (Ufunuo 16:15, NW)
-
-
Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye TamatiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
29, 30. (a) Ni nini kinachodokezwa na onyo la Yesu kwamba wale wanaopatikana wakilala wangeona aibu kwa kupoteza “mavazi ya nje” yao? (b) “Mavazi ya nje” yanamtambulisha mvaaji kuwa nini? (c) Mtu anaweza kupotezaje mavazi yake ya nje ya ufananisho, na tokeo likiwa nini?
29 Ingawa hivyo, ni nini kinachodokezwa na onyo la kwamba wale wanaopatikana wakilala wangeona aibu kwa kupoteza “mavazi ya nje” yao? Katika Israeli wa kale, kuhani au Mlawi yeyote aliyekuwa katika kazi ya lindo kwenye hekalu alikuwa na daraka zito. Waelezaji Wayahudi hutuambia kwamba ikiwa yeyote alikutwa akilala akiwa katika kazi kama hiyo, mavazi yake yangeweza kuvuliwa kutoka kwake na kuchomwa, hivi kwamba aliaibishwa hadharani.
30 Yesu anaonya hapa kwamba jambo kama hilo laweza kutukia leo. Makuhani na Walawi walikuwa kivuli cha ndugu wapakwa-mafuta wa Yesu. (1 Petro 2:9) Lakini kwa upanuzi onyo la Yesu linatumika vilevile kuhusu umati mkubwa. Hapa mavazi ya nje yanayorejezewa hutambulisha mvaaji kuwa Shahidi Mkristo wa Yehova. (Linga Ufunuo 3:18; 7:14.) Ikiwa wowote wanaruhusu mibano ya ulimwengu wa Shetani iwabembeleze walale usingizi au waingie ndani ya kutotenda, wao wanaelekea kupoteza mavazi ya nje, kwa maneno mengine, wapoteze utambulisho wao safi wa kuwa Wakristo. Hali kama hiyo ingekuwa yenye aibu. Ingemweka mmoja katika hatari ya kupoteza kabisa kila kitu.
-