-
Kukabiliana na HasaraAmkeni!—2002 | Machi 22
-
-
Kwa mfano, tetemeko la ardhi lilipoharibu jiji la Armenia lililoko magharibi mwa Kolombia mapema katika mwaka wa 1999, zaidi ya watu elfu moja walikufa, na wengine wengi walishtuka na kufadhaika. Roberto Estefan, daktari wa magonjwa ya akili ambaye nyumba yake iliharibiwa wakati wa msiba huo, alisema hivi: ‘Kokote uendako, watu wanaomba msaada. Ninapokwenda kula kwenye mkahawa, watu wengi wanaonisalimu wananieleza huzuni yao na jinsi wanavyoshindwa kulala.’
-
-
Kukabiliana na HasaraAmkeni!—2002 | Machi 22
-
-
Kuwasaidia Watu Waliofadhaika
Majanga yanapotokea, Mashahidi wa Yehova huwasaidia waokokaji kimwili, kiroho na kihisia. Kwa mfano, mara tu baada ya tetemeko la ardhi lililotajwa awali kutokea huko Kolombia, ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini humo ilianzisha halmashauri ya dharura kwenye eneo hilo. Maelfu ya Mashahidi kutoka sehemu zote za nchi hiyo walichanga chakula na fedha. Punde baadaye, tani 70 hivi za chakula zilitumwa kwenye eneo lililokumbwa na msiba.
Mara nyingi, watu wanahitaji sana msaada wa kiroho. Asubuhi moja baada ya tetemeko la ardhi kutokea huko Kolombia, Shahidi mmoja wa Yehova katika eneo hilo alimwona mwanamke aliyeonekana kuwa mwenye huzuni nyingi akitembea katika barabara moja ya jiji la Armenia lililokumbwa na msiba huo. Alimwendea mwanamke huyo na kumpa trakti yenye kichwa Kuna Tumaini Gani kwa Wapendwa Waliokufa?a
Mwanamke huyo alienda na trakti hiyo nyumbani na akaisoma kwa uangalifu. Baadaye, Shahidi mwingine wa Yehova alipomtembelea nyumbani kwake, mwanamke huyo alichochewa kusimulia mambo yaliyompata. Tetemeko hilo la ardhi lilikuwa limeharibu nyumba zake kadhaa katika jiji hilo ambazo zilikuwa zinamletea fedha nyingi. Sasa alikuwa ametumbukia katika umaskini. Lakini aliathiriwa hata zaidi. Tetemeko hilo lilibomoa nyumba yake ambamo yeye na mwanawe mwenye umri wa miaka 25 waliishi, na kumwua mwana huyo. Mwanamke huyo alimweleza Shahidi huyo kwamba hapo awali hakupendezwa kamwe na dini lakini sasa alikuwa na maswali mengi. Trakti hiyo ilikuwa imempa tumaini. Punde baadaye, alianza kujifunza Biblia.
-