Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya Wakristo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 28. Kunakuwa nini wakati malaika wa tatu anapopuliza tarumbeta yake?

      28 “Na malaika wa tatu akapuliza tarumbeta yake. Na nyota kubwa yenye kuwaka kama taa ikaanguka kutoka mbinguni, na ikaanguka juu ya theluthi moja ya mito na juu ya vibubujiko vya maji. Na jina la nyota linaitwa Pakanga. Na theluthi ya maji ikageuka kuwa pakanga, na wengi wa wanadamu wakafa kwa hayo maji, kwa sababu haya yalikuwa yamefanywa kuwa machungu.” (Ufunuo 8:10, 11, NW)

  • Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya Wakristo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 33. Ni mfichuo gani wa viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo uliofanywa kwenye mkusanyiko wa 1924 katika Kolumbasi, Ohaiyo, U.S.A.?

      33 Yenye kutokeza kuhusiana na hili ni ile mbiu iliyopigwa kwenye ule ambao gazeti The Golden Age liliueleza kuwa “mkusanyiko ulio mkubwa zaidi ya yote wa Wanafunzi wa Biblia uliofanywa wakati wa enzi zilizopita.” Mkusanyiko huu ulikusanyika katika Kolumbasi, Ohaiyo, Julai 20-27, 1924. Pasipo shaka kwa mwelekezo wa malaika ambaye alivumisha ile tarumbeta ya tatu, azimio lenye kujaa kani lilikubaliwa huko na baadaye nakala milioni 50 zikagawanywa zikiwa trakti. Lilitangazwa chini ya kichwa Viongozi wa Kidini Washtakiwa. Kichwa kidogo kilitoa suala hili: “Mbegu ya Ahadi Dhidi ya Mbegu ya Nyoka.” Shtaka lenyewe lilifichua waziwazi viongozi wa kidini juu ya mambo kama vile kujitwalia kwao wenyewe majina ya cheo ya kujiweka juu sana, kufanya kwao wanabiashara wakubwa-wakubwa na wanasiasa wa kulipwa kuwa ndio wakuu wa makundi yao, kutamani kwao kung’aa mbele ya watu, na kukataa kwao kuhubiria watu ujumbe wa Ufalme wa Mesiya. Lilikazia kwamba kila Mkristo aliye wakfu amepewa utume na Mungu atangaze “siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao.”—Isaya 61:2.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki