Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jamhuri Ya Kongo (Brazzaville)
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • Kweli Yaanza Kuwaweka Watu Huru

      Hebu sasa tuendelee na simulizi la Etienne. Alipokea kile kitabu mwaka wa 1947. Mara tu alipokipokea, Etienne alisoma sura kadhaa za kwanza na kuzizungumzia na jirani yake. Wote walitambua kwamba kinafundisha kweli na hivyo wakaamua kuwaalika rafiki zao Jumapili iliyofuata ili wakisome pamoja na kuchunguza maandiko yaliyomo. Wale waliofika walifurahia mambo waliyojifunza, wakaamua kukutana tena Jumapili iliyofuata. Afisa mmoja wa forodha anayeitwa Augustin Bayonne alihudhuria mkutano wa pili. Yeye pia alizaliwa Brazzaville kama Etienne, naye pia akawa mhubiri mwenye bidii wa kweli inayowaweka watu huru.

      Juma lililofuata, Etienne alipokea barua mbili. Moja ilitoka kwa mtu ambaye alimfahamu huko Kamerun, aliyejua kwamba Etienne alipendezwa na mambo ya dini. Alimweleza kwamba alikuwa ametuma jina la Etienne kwenye ofisi ya Watch Tower Society huko Uswisi. Barua ya pili ilitoka Uswisi na ilimwarifu Etienne kwamba alikuwa ametumiwa kitabu fulani na ilimtia moyo akisome na kuwaeleza familia na rafiki zake mambo aliyojifunza. Pia barua hiyo ilikuwa na anwani ya ofisi ya Ufaransa ambako angeweza kupata habari zaidi. Sasa Etienne alielewa ni kwa nini alitumiwa kitabu hicho. Baada ya muda alianza kuwasiliana kwa ukawaida na ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova huko Ufaransa.

      Baada ya miaka michache, Etienne na Augustin walirudi Brazzaville. Lakini kabla ya kurudi, Etienne alimwandikia Timothée Miemounoua, rafiki yake aliyekuwa msimamizi wa chuo cha ufundi huko Brazzaville. Alianza barua yake kwa kusema hivi: “Ninafurahi kukufahamisha kwamba tumekuwa tukifuata njia isiyo ya kweli. Mashahidi wa Yehova wana kweli.” Kisha Etienne akamweleza yale ambayo alikuwa amejifunza.

  • Jamhuri Ya Kongo (Brazzaville)
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • Hata hivyo, Ndugu Cooke hakujua Kifaransa. Etienne anasema hivi: “Akitumia kamusi yake ndogo ya Kiingereza na Kifaransa, ndugu huyo mnyenyekevu na mwenye fadhili alijitahidi sana kutueleza kuhusu tengenezo la Mungu na kazi ya kuhubiri juu ya Ufalme. Nyakati nyingine hatukumwelewa hata kidogo.”

  • Jamhuri Ya Kongo (Brazzaville)
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • [Picha katika ukurasa wa 139]

      Etienne Nkounkou

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki