Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Oktoba 15
    • Mbinu nyingine za tiba au upimaji zinazohusisha damu ya mtu mwenyewe hazipingani moja kwa moja na kanuni za Mungu. Kwa mfano, Wakristo wengi wameruhusu damu yao itolewe ili ipimwe au ichunguzwe, na baadaye damu hiyo inamwagwa. Mbinu nyingine tata zaidi zinazohusisha damu ya mtu mwenyewe zaweza pia kupendekezwa na daktari.

      Kwa mfano, wakati wa upasuaji fulani, huenda kiasi fulani cha damu kikatolewa mwilini kwa kutumia mbinu iitwayo hemodilution. Damu ya mgonjwa inayobaki inatiwa umajimaji. Baadaye, damu yake iliyo katika mzunguko wa damu wa nje inarudishwa katika mwili wake, hivyo kufanya kiasi cha damu yake kiwe karibu sawa na kile cha kawaida. Vivyo hivyo, damu inayotiririka kwenye kidonda inaweza kuchukuliwa na kuchujwa ili chembe nyekundu ziweze kurudishwa katika mwili wa mgonjwa; mbinu hii inaitwa uokoaji wa chembe za damu. Katika mbinu nyingine, damu inaweza kuelekezwa katika mashine ambayo kwa muda inafanya kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na viungo vya mwili (kwa mfano, moyo, maini, au mafigo). Kisha damu hiyo iliyo katika mashine irudishwe katika mwili wa mgonjwa. Katika mbinu nyingine, damu inaelekezwa katika chombo cha kuitenganisha (mashinepewa) ili sehemu zake zilizoharibika au zenye kasoro ziondolewe. Au lengo laweza kuwa kutenga sehemu fulani ya damu na kuitumia katika sehemu nyingine ya mwili. Pia kuna upimaji mwingine ambao kiasi fulani cha damu hutolewa ili kujua aina yake au kuichanganya na dawa, halafu inarudishwa katika mwili wa mgonjwa.

      Mbinu hizo zaweza kuwa tofauti, na bila shaka mbinu, matibabu, na upimaji mpya wa damu zitatokezwa. Si jukumu letu kuchanganua kila mbinu tofauti na kutoa uamuzi. Mkristo apaswa kuamua mwenyewe kuhusu jinsi damu yake mwenyewe itakavyotumiwa wakati wa upasuaji, upimaji damu, au tiba inayotumika wakati huo. Anapaswa kujua mapema kutoka kwa daktari au mtaalamu wa kitiba mambo ambayo huenda yakafanyiwa damu yake wanapotumia mbinu hiyo. Kisha lazima aamue kulingana na dhamiri yake. (Ona sanduku.)

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Oktoba 15
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 31]

      MASWALI UNAYOPASWA KUJIULIZA

      Ikiwa sehemu ya damu yangu itaelekezwa sehemu nyingine nje ya mwili wangu na mtiririko wake ukatishwe kwa muda, je, dhamiri yangu itaniruhusu kuona damu hiyo kuwa sehemu ya mwili wangu bado, hivyo nisihitaji ‘kuimwaga chini’?

      Je, dhamiri yangu iliyozoezwa kwa Biblia itanisumbua ikiwa wakati wa kupima ugonjwa au wa matibabu sehemu ya damu yangu itatolewa, iongezwe vitu vingine, na kurudishwa mwilini mwangu?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki