Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hicho Kitabu Kiliokokaje?
    Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote
    • Ili kutolea kielezi usahihi wa wanakiliji, fikiria Wamasora.a Kuhusu wao, msomi Thomas Hartwell Horne afafanua hivi: “Wao . . . walihesabu ni ipi iliyo herufi ya katikati ya Pentateuki [vitabu vitano vya kwanza vya Biblia], ni kipi kishazi cha katikati cha kila kitabu, na ni mara ngapi kila herufi ya alfabeti [ya Kiebrania] hutokea katika Maandiko yote ya Kiebrania.”3

      Hivyo, wanakiliji wastadi walitumia njia kadhaa za kuchunguza kutoka pande mbalimbali. Ili kuepuka kuacha herufi hata moja katika maandishi ya Biblia, walifikia hatua ya kuhesabu si maneno tu yaliyonakiliwa bali pia na herufi. Fikiria ule uangalifu mwingi uliohusika katika hilo: Yaripotiwa kwamba walihesabu herufi mojamoja 815,140 katika Maandiko ya Kiebrania!4 Jitihada hizo nyingi zilihakikisha usahihi wa kadiri ya juu.

  • Hicho Kitabu Kiliokokaje?
    Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote
    • a Wamasora (jina limaanishalo “Mabwana-Wakubwa wa Desturi”) walikuwa wanakiliji wa Maandiko ya Kiebrania walioishi kati ya karne ya sita na kumi W.K. Nakala za hati walizotokeza zinarejezewa kuwa maandishi ya Kimasora.2

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki