Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sehemu ya 4—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Wakati maombi ya visa ambazo zingewezesha wamishonari waliozoezwa Gileadi kutumikia katika Ivory Coast (sasa huitwa Côte d’Ivoire) yalipopelekwa, maofisa Wafaransa walikataa kutoa kibali. Hivyo, katika 1950, Alfred Shooter, kutoka Gold Coast (sasa ni Ghana), alitumwa kwenye jiji kuu la Ivory Coast akiwa painia. Mara alipoimarisha makao, mke wake akajiunga naye; na miezi michache baadaye, wenzi wa ndoa wamishonari, Gabriel na Florence Paterson, wakaja. Matatizo yakazuka. Siku moja, fasihi zao zilikamatwa kwa sababu hazikuwa na kibali cha serikali, nao ndugu wakapigwa faini. Lakini baadaye walipata vitabu vyao vikiuzwa sokoni, kwa hiyo wakavinunua na kuvitumia vizuri.

      Wakati huohuo, ndugu hao walitembelea ofisi nyingi za serikali katika jitihada ya kupata visa za kudumu. Bw. Houphouët-Boigny, aliyepata baadaye kuwa rais wa Ivory Coast, alijitolea asaidie. “Kweli,” akasema, “haina kizuizi chochote. Ni kama mto wenye nguvu nyingi; ujengee bwawa nao utafurika juu ya bwawa.” Wakati padri Mkatoliki na mhudumu Mmethodisti walipojaribu kutatiza, Ouezzin Coulibaly, ofisa mdogo wa serikali, akasema: “Mimi nawakilisha watu wa nchi hii. Sisi ndio watu, nasi twawapenda Mashahidi wa Yehova na kwa hiyo sisi twataka wakae katika nchi hii.”

  • Sehemu ya 4—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Picha katika ukurasa wa 478]

      Alipotishwa kufukuzwa nchini, Gabriel Paterson (anayeonyeshwa hapa) alipewa uhakikishio na ofisa mashuhuri: ‘Kweli ni kama mto wenye nguvu nyingi; ujengee bwawa nao utafurika juu ya bwawa’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki