Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ngono ya Simu Ina Ubaya Gani?
    Amkeni!—2004 | Februari 22
    • Hatari Wakati wa Uchumba

      Vipi kuhusu watu wanaochumbiana? Bila shaka ni jambo la kawaida kwa watu wanaopendana kutaka kuonyeshana upendo. Katika nyakati za Biblia, msichana mmoja aliyemwogopa Mungu alisema hivi kuhusu mchumba wake: “Mimi ni wa mpenzi wangu, na tamaa yake imenielekea mimi.” (Wimbo wa Sulemani 7:10) Siku ya arusi inapokaribia, inafaa watu walioamua kuoana wazungumzie mambo fulani mazito. Hata hivyo, je, ngono ya simu ndiyo njia salama ya kuonyesha hisia za mahaba?

      La. Hata wenzi ambao wameamua kufunga ndoa wanapaswa kufuata shauri hili la mtume Paulo: “Uasherati na ukosefu wa usafi wa kila namna au pupa visitajwe hata kidogo katikati yenu, kama inavyowafaa watu watakatifu; wala mwenendo wa aibu wala maneno ya kipumbavu wala mizaha michafu, mambo yasiyofaa, lakini badala ya hayo, utoaji wa shukrani. Kwa maana mnajua hili, nanyi mnalitambua wenyewe, kwamba hakuna mwasherati au mtu asiye safi au mtu mwenye pupa—maana yake ni kuwa mwabudu-sanamu aliye na urithi wowote katika ufalme wa Kristo na wa Mungu.”—Waefeso 5:3-5; Wakolosai 3:8.

      Ni wazi kwamba mazungumzo ya kimahaba yaliyokusudiwa kuamsha mawazo yaliyopotoka au yanayomchochea mtu kupiga punyeto ni machafu machoni pa Yehova. Hata yanaweza kumfanya mtu avunje kanuni za Mungu. Kwa mfano, wenzi fulani walikuwa wanachumbiana wakiwa sehemu mbalimbali. Mwanzoni waliwasiliana kwa simu mara nyingi ili wajuane vizuri. Hata hivyo, baada ya muda mfupi, wakaanza kuzungumzia mambo machafu. Mazungumzo yao yakawa machafu zaidi na zaidi. Basi, si ajabu kwamba walipokutana hatimaye, walifanya mambo machafu.

  • Ngono ya Simu Ina Ubaya Gani?
    Amkeni!—2004 | Februari 22
    • Iwapo umefunga uchumba, jitahidi kubaki safi, hata unapozungumza kwenye simu. Mwanamke mmoja Mkristo anayeitwa Leticia, ambaye anakaribia kufunga ndoa, anasema hivi: “Mimi na mchumba wangu tumesoma makala zinazotegemea Biblia kuhusu kudumisha usafi wa kiadili. Zimetusaidia kudumisha dhamiri safi.” Mazungumzo yanapoanza kuwa machafu, usiogope kuyabadili. Zungumzieni umuhimu wa kuwa na maongezi yanayofaa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki